Papa Felix III
Papa Felix III alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Machi 483 hadi kifo chake tarehe 25 Februari/1 Machi 492[1]. Alitokea Roma, Italia, katika ukoo maarufu.
Alimfuata Papa Simplicio akafuatwa na Papa Gelasio I.
Uamuzi wake wa kwanza ulikuwa kukataa hati maarufu kama Henotikon kwa sababu haikusema wazi kwamba Yesu Kristo ana hali mbili, Umungu na utu [2]. Uamuzi huo ulisababisha farakano la Acacius wa Konstantinopoli.
Upande wa Afrika Kaskazini aliamua suala la Wakatoliki waliokubali kubatizwa tena na Waario ili kukwepa dhuluma ya watawala Wavandali[3]. Kufuatana na sinodi maalumu ya mwaka 487 aliwaandika maaskofu wa huko masharti ya kuwapokea upya kundini[4][5].
Kutokana na watoto aliowazaa katika ndoa yake kabla hajachaguliwa, walipatikana baadaye Papa Agapeto I (mjukuu) na Papa Gregori I (kitukuu)[6][7].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 1 Machi[8][9].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
- Mababu wa Kanisa
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Monks of Ramsgate. "Felix III". Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 26 February 2017
- ↑ Victor of Vita, History of the Vandal Persecution, 2.3-6 (John Moorhead, trans.), Liverpool: University Press, 1992, p. 25
- ↑ "Pope Saint Felix III". New Catholic Dictionary. CatholicSaints.Info. 2 October 2015
- ↑ This article incorporates text from a publication now in the public domain: Coleman, Ambrose (1909). "Pope St. Felix III". In Herbermann, Charles. Catholic Encyclopedia. 6. Robert Appleton Company.
- ↑ Coleman, Ambrose. "Pope St. Felix III." The Catholic Encyclopedia. Vol. 6. New York: Robert Appleton Company, 1909. 6 Apr. 2013
- ↑ R.A. Markus, Gregory the Great and his world (Cambridge: University Press, 1997), p. 8
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
- ↑ "Pope Saint Felix III". 11 Oktoba 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Felix III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |