Sinodi
Sinodi (kwa Kiingereza "synod", kutoka maneno ya Kigiriki σύν, syun, "pamoja" na όδος, odos, "njia" = syunodos, yaani kufuata "njia ya pamoja", kwa hiyo "mkusanyiko" au "mkutano") ni mkutano wa Kanisa la Kikristo ambao huunganisha wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za Kanisa au eneo maalumu ndani ya Kanisa kama sinodi.
Kiasili sinodi ilikuwa mkutano wa maaskofu wa eneo fulani.
Wakati mwingine neno "mtaguso" hutumiwa kwa kutaja sinodi ya maaskofu wote, kwa mfano mtaguso mkuu ni mkutano wa maaskofu wote wa Kanisa Katoliki duniani.
Mara nyingi mkutano mkuu wa dayosisi au wa jimbo la Kanisa huitwa pia "sinodi".
Katika madhehebu ya Kiprotestanti sinodi hujumlisha wachungaji pamoja na walei.
Wapresbiteri hutumia neno "sinodi" kwa ajili ya mikoa yao ikitawaliwa na sinodi, yaani mkutano wa wajumbe kutoka shirika mbalimbali.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- GCatholic.org
- Pope Benedict holds first synod
- "Synod" at the Catholic Encyclopedia
- Synod of Diamper
- The synod of Constantinople in Byzantine times (in German) Archived 18 Januari 2012 at the Wayback Machine.
- Calculating the Synod? A network analysis of the synod of Constantinople in Late Byzantine times Archived 18 Januari 2012 at the Wayback Machine.
- Sobor in Encyclopedia of Ukraine
- Photograph of American sobor Archived 27 Septemba 2011 at the Wayback Machine.
- Synod of Bishops on the Family 2014 Archived 22 Aprili 2018 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sinodi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |