Papa Vitalian
Papa Vitalian alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Julai 657 hadi kifo chake tarehe 27 Januari 672[1]. Alitokea Segni, Lazio, Italia[2].
Jina la baba yake lilikuwa Anastasius[3].
Alimfuata Papa Eugenio I akafuatwa na Papa Adeodato II.
Kama Papa Eugenio I alijaribu kurudisha uhusiano mzuri na Dola la Roma Mashariki na Patriarki wa Konstantinopoli kuhusu uzushi uliofundisha kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu, lakini suala lilieleweka tu baadaye, katika Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli (680-681) uliolaani uzushi huo.
Alifaulu kuimarisha uhusiano na Wakristo wa Uingereza kupitia sinodi ya Whitby[4] na Theodoro wa Tarso[5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu yake tarehe 27 Januari[6], lakini Waorthodoksi tarehe 23 Julai.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ "Miranda, Salvatore. "The Cardinals of the Holy Roman Church", Florida International University". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-02. Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
- ↑ Sir Frank Stenton, Anglo-Saxon England, third edition (Oxford: Clarendon Press, 1971), pp. 123, 130
- ↑ Stenton, Anglo-Saxon England, p. 131
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Vitalian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |