Pata taarifa kuu

Marekani: Kamala Harris aahidi "kutokaa kimya" kuhusu Gaza baada ya mazungumzo na Netanyahu

Makamu wa rais wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris ametoa ishara hivi punde siku ya Alhamisi hii, Julai 25, 2024, ya uwezekano wa mabadiliko makubwa katika sera ya Marekani kuhusu Gaza, akiahidi kutosalia "kimya" mbele ya mateso ya raia na kusisitiza juu ya haja ya kuhitimisha makubaliano ya amani bila kuchelewa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akipokelewa na Makamu wa Rais wa Marekani na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris, Julai 25, 2024 mjini Washington.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akipokelewa na Makamu wa Rais wa Marekani na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris, Julai 25, 2024 mjini Washington. © Nathan Howard / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mbali na mazoea ya Rais anayemaliza muda wake Joe Biden, ambaye anapendelea shinikizo la nyuma ya pazia na Israeli, makamu wa rais ametangaza, baada ya kukutana na Benjamin Netanyahu, kwamba ulikuwa wakati wa kukomesha vita "mbaya".

"Kilichotokea Gaza katika muda wa miezi tisa iliyopita ni huzuni mtupu," amesema, akimaanisha "watoto waliouawa" na "watu waliokata tamaa na wenye njaa wanaokimbia kwa kuhofia usalama wao." "Hatuwezi kwenda mbali na majanga haya. Hatuwezi kumudu kutojali mateso na sitakaa kimya,” ameongeza mbele ya vyombo vya habari.

Seneta huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 59 na anahiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Ikulu ya White House baada ya kujiondoa kwa Joe Biden mwishoni mwa wiki iliyopita, ameelezea kwamba alisisitiza kwa Benjamin Netanyahu juu ya hali mbaya wakati wa mkutano huu wa "wazi". Alimtaka ahitimishe makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka na Hamas ili kumaliza vita vilivyochochewa na shambulio la kundi hili la Wapalistina dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7. Kamala Harris pia alitoa wito wa kuundwa kwa taifa la Palestina, jambo ambalo Waziri Mkuu wa Israel anapinga.

Hotuba ambayo inatofautiana na taswira ya upole iliyoonyeshwa na Joe Biden na Benyamin Netanyahu mapema siku hiyo, hata kama wawili hao wanadumisha mahusiano yenye utata. Ni katika hali ya msukosuko wa kisiasa ambapo Waziri Mkuu wa Israel alikanyaga Marekani, siku nne tu baada ya tangazo la kujiondoa kwa Joe Biden, 81, katika kampeni za uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

"Ningependa kuwashukuru kwa miaka hii 50 ya utumishi wa umma na msaada kwa taifa la Israeli," kiongozi huyo wa Israeli alisema kabla ya kuongeza: "Ninatarajia kufanya kazi nanyi katika miezi ijayo." Rais wa Marekani ameonyesha uungaji mkono wake mkubwa kwa Israel tangu kuanza kwa mzozo huo, lakini amekuwa akikosolewa kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wahanga wa raia katika Ukanda wa Gaza. Sasa anataka kuweka shinikizo kwa Benjamin Netanyahu kwa matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Ikulu ya White House ilieleza kuwa rais wa Marekani amethibitisha hitaji la kufikia makubaliano "haraka", kulingana na msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.