Pata taarifa kuu

Haiti: Makundi mawili yenye silaha yatia saini makubaliano ya kumaliza mvutano

Viongozi wa makundi mawili yenye silaha nchini Haiti wameripotiwa kutia saini makubaliano ya kumaliza mzozo.

Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa.
Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Haiti imekuwa ikikabiliwa na machufuko yanayotokana na makundi ya watu wenye silaha yanayowahangaisha raia, baadhi ya wangine wakitekwa.

Hali ilikuwa mbaya zaidi mwezi Februari baada ya watu wenye silaha kutekeleza shambulio katika mji mkuu wa Port-au-Prince wakiwa na nia ya kumtimua madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Ariel Henry.

Makundi yenye silaha yanaripotiwa kudhibiti sehemu kubwa ya taifa hilo ambapo yanatuhumiwa kwa kutekeleza mauaji, uporaji wa mali pamoja na utekaji wa raia ilikulipwa kikombozi.

Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakiyumbisha usalama nchini Haiti kwa kipindi kirefu.
Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakiyumbisha usalama nchini Haiti kwa kipindi kirefu. © Ralph Tedy Erol / Reuters

Kwa mujibu wa makubaliano hayo kati ya viongozi wa kundi la G9 na lile na G-Pep, vizuizi vya barabarani katika mji wa shantytown wenye karibia watu laki tatu viliondolewa.

Mchungaji Jean Enock Joseph, mwenye umaarufu katika eneo hilo, ameeleza kwamba makubaliano kama hayo yaliafikiwa mwaka wa 2023 kabla ya kuvunjika majuma kadhaa baadae.

Kama ilivyo kwa raia wengi katika mji wa  Port-au-Prince, wakazi wa Cite Soleil walikuwa wamezuiwa kutembea kwa uhuru katika mtaa wa mabanda  uliogawanywa katika mitaa zinazodhibitiwa na magenge hasimu kwa hofu ya kuathiriwa kwenye makabiliano.

Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi.
Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi. © REUTERS - Ralph Tedy Erol

Magenge ya G9 na G-Pep hayajaripotiwa kuingia katika makabiliano tangu Februari, walipojiunga na muungano ulioanzisha kumpindua Henry.

Jimmy "Barbecue" Cherizier, mkuu wa G9 na mmoja wa viongozi wa muungano huo, alisifu ujasiri wa viongozi wa genge la Cite Soleil siku ya Alhamisi.

Ghasia katika mji wa Port-au-Prince zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, na kuzua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Kenya imewatuma polisi wake kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kusaidia kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti.
Kenya imewatuma polisi wake kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kusaidia kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti. © Marckinson Pierre / AP

Takriban watu 600,000 wamekimbia makazi yao nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa, ongezeko la asilimia 60 tangu Machi.

Tangu kuondoka kwa Ariel Henry, mamlaka za mpito zimeundwa ili kuirejesha utulivu na uongozi thabiti kwenye taifa hilo.

Kenya inaoongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kujaribu kurejesha hali ya utulivu nchini Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.