Pata taarifa kuu

Benjamin Netanyahu aapa kuendelea na vita Gaza mbele ya Bunge la Marekani lililogawanyika

Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu alitoa hotuba Jumatano Julai 24 kwa Bunge la Marekani, zaidi ya miezi tisa baada ya shambulio la Hamas Oktoba 7 na kuanza kwa vita huko Gaza. Ziara yake ilikosolewa vikali, maelfu ya waandamanaji waliandamana mbele ya Ikulu, na Wwabunge na maseeta kutoka chma cha Democratic wakaamua kususia ziara ya mwanasiasa huyo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akizungumza katika mbele ya wabunge na maseneta katika makao makuu ya Bunge la Capitole huko Washington, Jumatano, Julai 24, 2024.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akizungumza katika mbele ya wabunge na maseneta katika makao makuu ya Bunge la Capitole huko Washington, Jumatano, Julai 24, 2024. © Julia Nikhinson / AP
Matangazo ya kibiashara

Benjamin Netanyahu alishangiliwa kwa muda mrefu alipoingia kwenye Bunge la Marekani na maafisa waliochaguliwa wa chama cha Republican. "Ili nguvu za ustaarabu zipate ushindi," nchi hizo mbili lazima "zisalie kuwa na umoja," amesema.

Amesema "anajiamini" kuhusu mafanikio ya juhudi za kuwakomboa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, kwa kuzingatia kwamba juhudi hizi "zinaweza kushangiliwa kwa mafanikio". Netanyahu alimshukuru sana mwenzake wa Marekani "kwa juhudi zake zisizotetereka" kwa niaba ya mateka. Waziri Mkuu wa Israel amesisitiza mbele ya wawakilishi waliochaguliwa wa Congress umuhimu wa kiungo kinachounganisha nchi hizo mbili.

"Hatujilindi isi peke yetu. Adui zetu ni adui zenu, vita vyetu ni vita vyenu, na ushindi wetu utakuwa ushindi wenu,” amesema, akiongeza kwamba Israeli itafanya “chochote kinachohitajika” “kurudisha usalama” kwenye mpaka wake wa kaskazini. Kiongozi huyo pia almehiriki "maono yake kwa Gaza," akisema kwamba "kuondolewa kwa kijeshi na kupotoshwa kwa Gaza" kunaweza "kusababisha mustakabali wa usalama, ustawi na amani."

Wakati wa hotuba yake, Benjamin Netanyahu aliikosoa Iran, akiita sera yake "mhimili wa ugaidi" ambao "unapinga Marekani, Israel na marafiki zetu wa Kiarabu." Si mgongano wa ustaarabu, bali ni mgongano kati ya ushenzi na ustaarabu,” amesema. Wanaharakati wanaoiunga mkono Gaza wameteuliwa kuwa "wajinga wenye manufaa wa Iran" na Waziri Mkuu, ambaye anahakikisha kwamba Tehran inafadhili maandamano haya.

Pia alimsifu Rais wa zamani Donald Trump kwa kuendeleza Mkataba wa Abraham na kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, "mji mkuu wa milele na usiogawanyika." Anadumisha uhusiano mzuri sana na rais huyo wa zamani wa Marekani na akalaani jaribio la mauaji "la kuchukiza" ambalo lililenga mgombea wa chama cha Republican mnamo Julai 13.

Katika mkesha wa mkutano wake na Joe Biden, Benyamin Netanyahu anamshukuru kwa msaada wake kwa Israel, lakini anaongeza kuwa nchi yake inahitaji zana, yaani silaha, haraka zaidi, ili kumaliza kazi hiyo kwa haraka zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.