Wolfgang Amadeus Mozart
Wolfgang Amadeus Mozart (Salzburg, 27 Januari 1756 – Vienna, 5 Disemba 1791) alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria.
Licha ya kuwa na maisha mafupi (alifariki akiwa na umri wa miaka 35 tu), alitunga zaidi ya nyimbo 800 za kila aina, zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte (Filimbi ya Ajabu). Watu wanaamini kwamba Mozart ni moja kati ya watunzi bora wa muda wote wa nyimbo za Ulaya, ikimpelekea mtunzi mwenzake Joseph Haydn kuandika kuwa: "kizazi kingine hakitaona talanta kama yake tena kwa karne moja".
Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem, ambacho alikiacha hajakimaliza.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Familia na miaka ya mwanzoni
[hariri | hariri chanzo]Mozart alizaliwa katika familia ya wanamuziki. Baba yake, Leopold Mozart, alikuwa mpiga zeze na mtunzi mashuhuri ambaye alifanya kazi na Askofu mkuu wa Salzburg. Alikuwa na dada mkubwa, Maria Anna, aliyeitwa kwa jina la utani "Nannerl" (kulikuwa na ndugu wengine ambao walifariki wakiwa watoto).
Mozart alibatizwa asubuhi baada ya kuzaliwa kwake kwenye kanisa kuu la mjini Salzburg. Jina lake kamili kwa Kilatini lilikuwa “Joannes Chrysostomus Wolfgangus Theophilus Mozart”. Kwa kawaida alikuwa akifahamika kama “Wolfgang Amadeus Mozart”, na jina lake la utani lilikuwa “Wolfi”.
Nyumba alipozaliwa katika mtaa unaoitwa Getreidegasse, sasa hivi ni sehemu ya maonyesho ya Mozart.
Mozart alikuwa mtoto wa ajabu: tangu akiwa mdogo alikuwa na kipaji cha muziki ambacho si cha kawaida. Baba yake alimpa ala kadhaa ili amfundishe mwanawe kutunga muziki.
Wolfgang alijifunza kupiga kinanda akiwa na umri wa miaka mitatu, na baada ya muda mfupi akajifunza pia kupiga zeze na organo vilevile.
Kuna vipande viwili vifupi vya noti za piano alizotunga akiwa na umri wa miaka mitano, lakini ziliandikwa kwa mwandiko wa baba yake, hivyo si rahisi kusema kiasi cha msaada alioweza kuupata.
Baadaye baba yake akaanza kumruhusu mtoto wake, na kumfanya aanze kupiga kazi kwenye kumbi huku kukiwa na watu muhimu kibao mbele yake. Siku hizi hili linaweza kuitwa “ukandamizaji” wa watoto wenye vipaji, lakini miaka hiyo watu walikuwa hawaoni tatizo kumwachia mtoto atumike kwa namna hii. Inaonekana kwamba hili halikumwathiri kabisa, na hivyo akajikuta anakua akiwa mtunzi mkubwa kama vile alivyostahili kuwa.
Mozart alianza kupiga kwenye umma mjini Salzburg alipokuwa na umri wa miaka mitano, halafu akachukuliwa na kuelekea jijini Vienna akiwa na umri wa miaka sita.
Pia aliwahi kupiga mjini Linz na Pressburg (leo hii inaitwa Bratislava). Aliwahi kupiga mara mbili mbele ya malkia Maria Theresa wa Austria. Katika konseti hili alipiga nyimbo ambazo hata watu wazima wanaweza kuzicheza, na muziki ambao watu hawakuwahi kuusikia. Alikuwa akibuni mitindo na kuicheza huku akiwa amevaa kinanda, au akiwa hatazami mikono yake inapiga wapi na akipitisha mikono huku na huku. Pia alitengeneza miziki ambayo inafuata milio ya vitu vingine na alikuwa akiziweka mbeleni kwake.
Watu wengi walimsikia kijana huyu mashuhuri na kuandika habari zake na ndiyo maana hadi leo hii tunajua mengi yaliyotokea. Pia inajulikana kwamba alikuwa anaweza kukumbuka noti za muziki aliotunga akizichungulia mara moja tu.
Safari za kwanza nchi za nje
[hariri | hariri chanzo]Kwa muda mfupi Mozart akawa anasafiri nchi za nje kwa shughuli za kimuziki. Aliwahi kutumbuiza Munich, Prague, Paris, The Hague na London. Huko mjini London, alipiga mbele ya mfalme George III na kubahatika kukutana na mtunzi mmoja aitwaye Johann Christian Bach, mmoja kati ya watoto wa Johann Sebastian Bach. Alipenda sana muziki wa Christian Bach na hata akaamua kufanya pamoja naye kazi ya muziki.
Mnamo mwaka 1767 alikuwa zake mjini Vienna tena ambapo alipata ugonjwa wa ndui, lakini alipona, na baba yake aliona hili kama ni dalili kutoka kwa Mungu kwamba mtoto wake atakuwa salama.
Baada ya hapo akaenda nchini Italia ambapo alipata kusikia miziki ya watunzi wengine wengi wa Kiitalia. Watunzi hao ni pamoja na Gregorio Allegri ambaye aliandika wimbo Miserere ambao uliandikwa kwa ajili ya Papa na kwa kuimbiwa na kwaya nzima ya Basilika la Mt. Petro (Vatikani).
Katika tungo hizo, hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuona kilichoandikwa kwenye muziki huo, hivyo hakukuwa na mtu mwingine aliyeweza kuziimba katika kwaya. Cha kushangaza Mozart alizisikia mara moja tu na kukaa chini na kuzichezea kwa kutumia kumbukumbu yake tu!
Alikutana na Papa na kupewa naye knighthood ya Order of the Golden Spur.
Mnamo mwaka 1777, alikwenda safari akiwa na mama yake.
Huko Mannheim akatokea kumpenda msichana mmoja aliyeitwa Aloysia Weber. Alikuwa na umri wa miaka 16 tu na alikuwa akisomea kuimba. Mozart akataka amchukue kisha aende naye Italia ili amfanye maarufu, lakini baba yake akamwandikia barua kali ya mkwara wa kumtaka aache kufikiria huo upuuzi.
Kunako 1778, Mozart na mama yake walikuwa mjini Paris, lakini wakiwa huko mama akafariki dunia.
Mozart mjini Vienna
[hariri | hariri chanzo]Mozart aliandika opera ndogondogo kadhaa akiwa bwana mdogo, lakini opera yake ya kwanza na muhimu ilikuwa Idomeneo, ambayo ilianza kutumbuizwa mjini Munich mnamo 1780.
Mwaka uliofuatia akaenda zake Vienna. Lakini muda huo alikuwa akifanya kazi, kama baba yake, kwa Askofu Mkuu wa Salzburg. Aliporudi tena Salzburg akalumbana na Askofu Mkuu, kitendo ambacho kilipelekea kumfanya atimuliwe mbali. Mozart akarudi tena mjini Vienna ambapo alitumia maisha yake yote yaliyombakia.
Mnamo mwaka 1782, alimwoa Constanze Weber, mmoja kati ya wadogo watatu wa Aloysia (ambaye kwa wakati huo alikuwa ameolewa na mtu mwingine). Walibarikiwa kupata watoto saba, lakini kwa bahati mbaya watano kati yao walikufa wakiwa bado wadogo. Baba yake Mozart hakupitisha ndoa hiyo. Constanze alikuwa mke mpendwa, lakini, kama Mozart, hakuwa mzuri sana katika suala la kutafuta fedha, hivyo mara nyingi walikuwa maskini.
Mwaka huohuo 1782, Mozart akatunga opera nyingine iliyompa mafanikio makubwa kabisa: Die Entführung aus dem Serail ("Kutekwa nyara kutoka Seraglio"). Ni hadithi moja maarufu inayoelezea kwamba, baada ya mtawala kusikia opera, akamwuliza Mozart kama kulikuwa na “noti nyingi?”. Mozart akamjibu yule mtawala: “Zipo kiasi cha zitakazotakikana, Mtukufu.”
Tangu hapo, Mozart akaanza kutumbuiza katika makonseti mfululizo akipiga piano yake mwenyewe, iliyokuwa ikielekezwa kutoka kwenye kinanda.
Katika safari zake akapata kukutana na mtunzi mwenzi Joseph Haydn na hao watu wawili wakawa marafiki wakubwa; mara nyingi walipiga pamoja kwenye string quartet. Siku moja Haydn aliyasema haya kwa Leopold Mozart: "Mbele ya Mungu na nikiwa msemakweli ni kwamba mtoto wako ni mtunzi mkubwa anayejulikana nami kibinafsi au kijina. Ana ladha, na cha zaidi ni kwamba, mtu mwenye uelewa mkubwa katika utunzi."
Mozart alikuwa mwanachama wa Masonic Lodge kama alivyokuwa Haydn, na alitengeneza kazi kadhaa kwa ajili yake.
.
Mozart huko Prague
[hariri | hariri chanzo]Baada ya muda fulani watazamaji wengi wa mjini Vienna hawakuwa wakimwunga mkono sana Mozart, hivyo mara nyingi alienda zake mjini Prague mahali ambapo washabiki wengi walikuwa wakimpenda. Opera yake Ndoa ya Figaro ilikuwa maarufu sana kule, na mwaka 1787 akatumbuiza kwa mara ya kwanza opera yake Don Giovanni.
Kuumwa na kufa kwake
[hariri | hariri chanzo]Kuna hadithi chungu nzima zinazohusu ugonjwa wa mwisho na kifo cha Mozart, na si rahisi kuwa na hakika ya kipi hasa kilitokea.
Alikuwa akifanya kazi kwenye opera The Magic Flute ambayo ni moja kati ya kazi zake kubwa na ni maarufu sana hadi leo hii. Opera hiyo iliandikwa kwa Kijerumani, na si kwa Kiitalia, kama ilivyo kwa opera zake nyingine nyingi. Katika hali nyingine ipo kama Kiingereza hivi pantomime.
Wakati huohuo aliokuwa akifanya kazi hii akaombwa na mtu mmoja atunge kwa siri requiem (maombi kwa ajili ya marehemu). Pia akaombwa atunge opera ya Kiitalia La Clemenza di Tito. Hii iliimbwa mjini Prague wakati wa Septemba mwaka 1791. Mwishoni kabisa mwa mwezi huo The Magic Flute ilipigwa kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo Mozart akawa anashughulikia vilivyo Requiem.
Alipata kugundua kwamba tayari yu mgonjwa sana, na kwa maana hiyo ile requiem ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe. Alikufa kabla hajaweza kuimaliza. Constanze akamwomba mtunzi mwingine, aliyeitwa Franz Xaver Süssmayr, kuimalizia kazi. Hadi leo hii hatuna hakika ni kipi kidogo alichoongezea Süssmayr, lakini yamkini karibu muziki wote ulikuwa kazi ya Mozart mwenyewe.
Mozart alizikwa kwenye kaburi lisilojulikana kwa sababu kulikuwa hakuna fedha za kutayarishia mazishi mazuri.
Muziki wa Mozart
[hariri | hariri chanzo]Muziki wa Mozart, kama ule wa Joseph Haydn, ni muziki mashuhuri sana unaojulikana kama Staili ya klasiki. Wakati huo alipoanza kutunga, kipindi cha muziki wa Baroque kilikuwa kinaelekea ukingoni. Ladha za muziki zilianza kupatikana katika muziki. Mozart alikuwa mtunzi wa kwanza kutunga muziki wa kutumia piano, kifaa pekee kilichokuwa kinakuja kuwa maarufu.
Alianza karibu kila aina ya muziki: symphonies, operas, solo concertos, chamber music, hasa string quartets na string quintets, na piano sonata. Pia, aliandika miziki kibao ya kidini, ikiwemo mass, na vilevile miziki mashuhuri kama vile dansi, divertimenti na serenade.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Abert, Hermann (2007). W. A. Mozart. Cliff Eisen (ed.), Stewart Spencer (trans.). New Haven: Yale University Press. ISBN 978-0-300-07223-5. OCLC 70401564.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Barry, Barbara R (2000). The Philosopher's Stone: Essays in the Transformation of Musical Structure. Hillsdale, New York: Pendragon Press. ISBN 1-57647-010-5. OCLC 466918491.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Braunbehrens, Volkmar (1990). Mozart: Lebensbilder. G. Lubbe. ISBN 978-3785705803.
- Deutsch, Otto Erich (1965). Mozart: A Documentary Biography. Peter Branscombe, Eric Blom, Jeremy Noble (trans.). Stanford: Stanford University Press. ISBN 978-0-8047-0233-1. OCLC 8991008.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Einstein, Alfred (1965). Mozart: His Character, His Work. Galaxy Book 162. Arthur Mendel, Nathan Broder (trans.) (tol. la 6th). New York City: Oxford University Press. ISBN 0-304-92483-0. OCLC 456644858.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Eisen, Cliff. "Mozart". Grove Music Online Kigezo:Subscription required. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2010.
{{cite journal}}
: Invalid|ref=harv
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Fradkin, Robert A. (1996) The well-tempered announcer: a pronunciation guide to classical music. Bloomington: Indiana University Press. ISBN 0-253-21064-X.
- Freeman, Daniel E. (2013). Mozart in Prague. Minneapolis: Bearclaw. ISBN 978-0-9794223-1-7.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Halliwell, Ruth (1998). The Mozart Family: Four Lives in a Social Context. New York City: Clarendon Press. ISBN 978-0-19-816371-8. OCLC 36423516.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - (Kijerumani) Haberl, Dieter (2006). "Beethovens erste Reise nach Wien: die Datierung seiner Schülerreise zu W. A. Mozart". Neues Musikwissenschaftliches Jahrbuch (14). OCLC 634798176.
{{cite journal}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Heartz, Daniel (2003). Music in European Capitals: The Galant Style, 1720–1780 (tol. la 1st). New York City: W. W. Norton & Company. ISBN 0-393-05080-7. OCLC 50693068.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Landon, Howard Chandler Robbins (1990). 1791: Mozart's Last Year. London: Flamingo. ISBN 978-0-00-654324-4. OCLC 20932333.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Lorenz, Michael (9 Agosti 2010). "Mozart's Apartment on the Alsergrund". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-01. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2010.
{{cite web}}
: Invalid|ref=harv
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - March, Ivan; Greenfield, Edward; Layton, Robert (2005). Czajkowski, Paul (mhr.). Penguin Guide to Compact Discs And DVDs, 2005–2006 (tol. la 30th). London: Penguin. ISBN 0-14-102262-0. OCLC 416204627.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Mozart, Wolfgang; Mozart, Leopold (1966). Anderson, Emily (mhr.). The Letters of Mozart and his Family (tol. la 2nd). London: Macmillan. ISBN 0-393-02248-X. OCLC 594813.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - "Mozart, Mozart's Magic Flute and Beethoven". Raptus Association for Music Appreciation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-11-27. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Rosen, Charles (1998). The Classical Style: Haydn, Mozart, Beethoven (tol. la 2nd). New York City: W. W. Norton & Company. ISBN 0-393-31712-9. OCLC 246977555.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Sadie, Stanley, mhr. (1998). The New Grove Dictionary of Opera. New York: Grove's Dictionaries of Music Inc. ISBN 978-0-333-73432-2. OCLC 39160203.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Sadie, Stanley, mhr. (1980). The New Grove Dictionary of Music and Musicians (tol. la 6th). London: Macmillan. ISBN 0-333-23111-2. OCLC 5676891.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Eisen, Cliff; Sadie, Stanley. "Mozart, Wolfgang Amadeus", in: The New Grove Dictionary of Music and Musicians, 2nd edition, vol. 17, ed. Stanley Sadie, Oxford University Press, Inc., New York, 2001. ISBN 978-0195170672.
- Solomon, Maynard (1995). Mozart: A Life (tol. la 1st). New York City: HarperCollins. ISBN 978-0-06-019046-0. OCLC 31435799.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Steptoe, Andrew (1990). The Mozart-Da Ponte Operas: The Cultural and Musical Background to Le nozze di Figaro, Don Giovanni, and Così fan tutte. Oxford: Clarendon Press. ISBN 0-19-816221-9. OCLC 22895166.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - "Award of the Papal Equestrian Order of the "Golden Spur" to Wolfgang Amadeus Mozart". Vatican Secret Archives. 4 Julai 1770. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-18. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Wakin, Daniel J.. "After Mozart’s Death, an Endless Coda", The New York Times, 24 August 2010.
- Wilson, Peter Hamish (1999) The Holy Roman Empire, 1495–1806. London: MacMillan Press.
- Wolff, Christoph (2012) Mozart at the Gateway to His Fortune: Serving the Emperor, 1788–1791. New York: Norton. ISBN 978-0393050707
Kujisomea zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Cairns, David (2006). Mozart and His Operas. Berkeley, California: University of California Press. ISBN 0-520-22898-7. OCLC 62290645.
- Eisen, Cliff; Keefe, Simon P, whr. (2006). The Cambridge Mozart Encyclopedia. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-85659-0. OCLC 60245611.
- Gutman, Robert (2000). Mozart: A Cultural Biography. London: Harcourt Brace. ISBN 978-0-15-601171-6. OCLC 45485135.
- Holmes, Edward (2005). The Life of Mozart. New York: Cosimo Classics. ISBN 1-59605-147-7. OCLC 62790104.
- Mozart, Wolfgang (1972). Mersmann, Hans (mhr.). Letters of Wolfgang Amadeus Mozart. New York: Dover Publications. ISBN 0-486-22859-2. OCLC 753483.
- "New Mozart Pieces Unveiled (Video)". The Huffington Post. 8 Februari 2009. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Till, Nicholas (1995). Mozart and the Enlightenment: Truth, Virtue and Beauty in Mozart's Operas. New York City: W. W. Norton & Company. ISBN 0-393-31395-6. OCLC 469628809.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Angalia mengine kuhusu Wolfgang Amadeus Mozart kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
- Salzburg Mozarteum Foundation
- Chronological-Thematic Catalog Ilihifadhiwa 26 Machi 2014 kwenye Wayback Machine.
- Shughuli au kuhusu Wolfgang Amadeus Mozart katika maktaba ya WorldCat catalog
- Digitized, scanned material (books, sheet music)
- "Mozart" Titles; Mozart as author from archive.org
- "Mozart" Titles; Mozart as author from books.google.com
- Digital Mozart Edition Ilihifadhiwa 18 Februari 2017 kwenye Wayback Machine. (Internationale Stiftung Mozarteum)
- (Kifaransa) "Mozart" titles from Gallica
- From the British Library
- Mozart's Thematic Catalogue Ilihifadhiwa 7 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine. (view with "Turning the Pages" Ilihifadhiwa 28 Septemba 2013 kwenye Wayback Machine.)
- Mozart's Musical Diary Ilihifadhiwa 24 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Background information on Mozart and the Thematic Catalogue Ilihifadhiwa 14 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine.
- (Kijerumani) Letters of Leopold Mozart und Wolfgang Amadeus Mozart Ilihifadhiwa 22 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine. (Badische Landesbibliothek)
- Muziki ya kuchapishwa
- Complete sheetmusic (scores) from the Neue Mozart-Ausgabe (Internationale Stiftung Mozarteum)
- "Mozart" Titles from the Munich Digitisation Centre (MDZ)
- "Mozart" Titles from the University of Rochester
- Wolfgang Amadeus Mozart ame orodheshwa katika International Music Score Library Project
- Free scores by Wolfgang Amadeus Mozart katika Choral Public Domain Library (ChoralWiki)
- Free typeset sheet music of Mozart's works from Cantorion.org