Mwana wa Daudi
Mandhari
Mwana wa Daudi ni jina la heshima la wanaume waliotokana na vizazi vya mfalme Daudi na hivyo kuhusishwa na ahadi alilopewa na nabii Nathani kwamba ukoo wake utatawala milele (2Sam 7:1-29).
Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika kwa Yesu aliyetambuliwa na wengi kuwa ndiye Masiya aliyetazamiwa, ama wakati wa maisha yake au baada ya kifo chake.
Injili ya Mathayo na Injili ya Luka zinasisitiza haki ya Yesu kuitwa hivyo kwa kuorodhesha vizazi kati ya Daudi na Yosefu, mume wa Bikira Maria, mama yake.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwana wa Daudi kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |