Gottlieb Daimler
Mandhari
Gottlieb Daimler (17 Machi 1834 – 6 Machi 1900) alikuwa mhandisi kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1885 alibuni injini ya petroli kwa ajili ya magari na vyombo vinginevyo. Hii ilikuwa injini ya petroli ya kwanza iliyokuwa ndogo na kuzunguka haraka. Baada ya kuanzisha kampuni yake ya binafsi, aliuza motokaa ya kwanza mwaka wa 1892.
Kampuni yake iliunganishwa baadaye na ile ya Karl Friedrich Benz kutengeneza magari mashuhuri ya Daimler-Benz.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gottlieb Daimler kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |