Nenda kwa yaliyomo

Ujerumani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Germany)
Bundesrepublik Deutschland
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Bendera ya Ujerumani Nembo ya Ujerumani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Einigkeit und Recht und Freiheit
(Kijerumani: "Umoja na Haki na Uhuru”)
Wimbo wa taifa: Wimbo wa Wajerumani (beti ya tatu)
Umoja na Haki na Uhuru
Lokeshen ya Ujerumani
Mji mkuu Berlin
52°31′ N 13°24′ E
Mji mkubwa nchini Berlin
Lugha rasmi Kijerumani 1
Serikali
Rais
Chansella (Waziri Mkuu)
Shirikisho la Jamhuri
Frank-Walter Steinmeier
Olaf Scholz
Dola Takatifu la Kiroma

Dola la Ujerumani
Shirikisho la Jamhuri
Maungano
843 (Mkataba wa Verdun)

18 Januari 1871
23 Mei 1949
3 Oktoba 1990
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
357,050 km² (ya 63)
2.416
Idadi ya watu
 - 2022 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
84,270,625 (ya 19)
80,219,695
232/km² (ya 58)
Fedha Euro (€) 2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .de
Kodi ya simu +49
1 Kideni, Kijerumani cha Kaskazini, Kisorbia, Kifrisia ni lugha rasmi katika mikoa kadhaa 2 hadi 1999: Mark (DM)


Ramani ya nchi
Lango la Berlin
Kanisa kuu la Köln
Ruegen-kreidefelsen

Ujerumani (pia: Udachi, kwa Kijerumani: Deutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.

Imepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.

Ndiyo nchi yenye watu wengi zaidi katika Ulaya, isipokuwa Urusi.

Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote duniani.

Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.

Jina la nchi

Wenyeji wanaiita nchi "Deutschland" (De-Deutschland.ogg Deutschland (info), tamka: doich-land) na jina hilo limeingia katika Kiswahili kama "Udachi". Lilikuwa jina la kawaida katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

Siku hizi neno "Ujerumani" limechukua nafasi yake kutokana na Kiingereza kinachoiita "Germany". Watu wengine hulichukua "Udachi" kuwa na maana "Uholanzi" wakilichanganya na neno la Kiingereza "Dutch" (tamka datsh) linalomaanisha "Kiholanzi".[1]

Jiografia

Ujerumani unaenea kati ya Bahari ya Kaskazini halafu ya Bahari Baltiki upande wa kaskazini na milima ya Alpi upande wa kusini. Mpaka na Denmark inakata sehemu ya kusini ya rasi ya Jutland. Mpaka wa kusini unafuata sehemu za chini za Alpi, Ziwa la Konstanz na mto Rhein dhidi ya Austria na Uswisi.

Mipaka yake upande wa magharibi na mashariki ilibadilika mara nyingi katika historia yake; baada ya vita kuu mbili za karne ya 20 maeneo makubwa yalitengwa na Ujerumani na kuwa sehemu za Poland, Urusi, Ucheki na Ufaransa. Wakazi Wajerumani kwa mamilioni walifukuzwa au kuwa raia wa nchi hizo.

Tangu mwaka 1945 mpaka wa mashariki ni mto Oder dhidi ya Poland na vilele vya Milima ya Madini (jer. Erzgebirge) na Msitu wa Bohemia.

Upande wa magharibi mpaka na Ufaransa ni mto Rhein pamoja na vilima kati ya Alsasi na Rhine-Palatino na vilima dhidi ya Luxemburg na milima ya Eifel dhidi ya Ubelgiji. Mpaka na Uholanzi katika magharibi kaskazini inapita katika tambarare ikifuata mistari ya kihistoria.

Ujerumani ina kanda tatu za kijiografia:

Tambarare ya pwani ya kaskazini ni eneo bapa; hakuna milima na nchi haipandi juu ya mita 200, sehemu kubwa ni kati ya uwiano wa bahari na mita 60 juu yake. Uso wa nchi ni tokeo la kupitiwa na barafuto kubwa za enzi ya barafu iliyopita iliyonyosha uso wa nchi ikiacha vilima vya mchanga, kokoto na ardhi ambavyo ni miinuko pekee inayofika hadi mita 200 juu ya uwiano wa bahari.

Nyanda za milima ya kati ni mabaki ya milima ya kale iliyotokea miaka milioni 350 iliyopita na kupungua sana tangu zamani zile kwa njia ya mmomonyoko. Kwa hiyo hakuna vilele vikali bali vyote vina umbo poa.

Alpi katika kusini ni milima mirefu Ujerumani ingawa sehemu kubwa na za juu zaidi ziko nje ya mipaka ya Ujerumani huko Ufaransa, Italia, Uswisi na Austria. Milima hiyo ilianza kutokea miaka 135-50 milioni iliyopita tu. Kilele cha juu katika Ujerumani ni mlima wa Zugspitze yenye urefu wa mita 2,962 juu ya UB.

Historia

Ugawaji wa Ujerumani mwaka 1945; Njano-nyeupe: maeneo yaliyotengwa na Ujerumani na kuwa sehemu za Poland na Umoja wa Kisovyeti, pamoja na kufukuza wakazi; nyekundu: mamlaka ya Kirusi (1949 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, kibichi: mamlaka ya Kiingereza, buluu: mamlaka ya Kifaransa (pamoja eneo la Saar mpakani mwa Ufaransa); kichungwa: mamlaka ya Kimarekani; maeneo ya mamlaka ya Kiingereze, Kifaransa na Kimarekani yalikuwa 1949 Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Makabila mbalimbali ya Wagermanik yamekuwa yakiishi kaskazini mwa Ujerumani wa leo tangu zamani za Roma ya Kale. Eneo lililoitwa kwa Kilatini "Germania" linajulikana tangu mwaka 100 BK.

Kuanzia mwaka 400 hivi, wakati wa Dola la Roma kudhoofika, makabila hayo yalisambaa hasa kwenda kusini.

Mnamo mwaka 800 Karolo Mkuu, mtawala wa Wafaranki, aliunganisha maeneo ya Ujerumani na Ufaransa ya leo akaendelea kutwaa Italia ya Kaskazini na ya Kati hadi Roma. Mwaka 800 Papa alimpa cheo cha "Kaisari wa Roma". Baada ya kifo chake himaya iligawanyika, na upande wa mashariki hatimaye viongozi wa makabila walikutana mwaka 919 wakamchagua mfalme kati yao anayehesabiwa kuwa mfalme wa kwanza wa Wajerumani.

Kuanzia karne ya 10 wafalme wa Ujerumani walikuwa pia wadhamini wa Papa wa Roma aliyeendelea kuwapa cheo cha "Kaisari". Hivyo himaya yao iliitwa Dola Takatifu la Kiroma.[2]

Katika karne ya 16 maeneo ya Ujerumani kaskazini yakawa kiini cha Matengenezo ya Kiprotestanti katika Ukristo.

Baada ya Dola Takatifu kusambaratika, Shirikisho la Ujerumani ulianzishwa mwaka 1815.

Mwaka 1871, Ujerumani ukawa taifa-dola chini ya Prussia.

Kisha kushindwa katika vita vikuu vya kwanza, hilo Dola la Ujerumani lilikoma na kuiachia nafasi Jamhuri ya Weimar.

Adolf Hitler aliposhika uongozi wa nchi mwaka 1933 aligeuza nchi kuwa ya kidikteta na kuingiza dunia katika vita vikuu vya pili ambapo hasa Wayahudi waliangamizwa kwa mamilioni katika makambi maalumu.

Baada ya kushindwa tena vitani, nchi iligawanyika pande mbili, magharibi chini ya Marekani, Uingereza na Ufaransa, na mashariki chini ya Muungano wa Kisovyeti.

Ukomunisti ulipopinduliwa mwaka 1989, tarehe 3 Oktoba 1990 Ujerumani mashariki ulijiunga na shirikisho la Ujerumani magharibi ambao ulikuwa tayari kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya wa leo.[3]

Katika karne ya 21 Ujerumani ni nchi ya kidemokrasia yenye maendeleo makubwa hasa upande wa uchumi.

Kuhusiana na hatua hizo mbalimbali za historia yake ndefu, inafaa kusoma pia:

Majimbo

  1. Baden-Württemberg
  2. Bavaria (Freistaat Bayern)
  3. Berlin
  4. Brandenburg
  5. Bremen (Freie Hansestadt Bremen)
  6. Hamburg (Freie und Hansestadt Hamburg)
  7. Hesse (Hessen)
  8. Mecklenburg-Pomerini (Mecklenburg-Vorpommern)
  9. Saksonia Chini (Niedersachsen)
  10. Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)
  11. Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)
  12. Saar (Saarland)
  13. Saksonia (Freistaat Sachsen)
  14. Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)
  15. Schleswig-Holstein
  16. Thuringia (Freistaat Thüringen)

Miji

Majiji yenye wakazi zaidi ya milioni moja ni:

Miji mikubwa mingine ni:

Watu

Wakazi ni Wajerumani asilia (76.4%), Wazungu wengine (11%), Waturuki (3.4%), Waasia wengine (3.5%, hasa kutoka Mashariki ya Kati), Waafrika (0.8%) n.k. Kati yao, 12% si raia wa nchi.

Lugha asilia ni Kijerumani kinachojadiliwa kwa lahaja mbalimbali, lakini wenyeji wote wanasikilizana. Katika maeneo mawili kuna wasemaji asilia wa Kideni na Kisorbia.

Wahamiaji wa karne ya 20 wameleta lugha zao, hasa Kituruki na lugha za Ulaya ya Kusini.

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, Wakristo ni 66.8% (Wakatoliki 30.8%, Walutheri 30.3%, Waprotestanti wengine 5.7%), huku Waislamu wakiwa 1.9%. Thuluthi moja ya wakazi haina dini yoyote. Kadirio la mwaka 2021 linasema Wakristo ni 52.7% (Wakatoliki 26%, Waprotestanti 23.7%, Waorthodoksi 1.9%, wengineo 1.1%), Waislamu walau 3.6%, Wabudha 0.3%, Wahindu 0.1%, Wayahudi 0.1%, Wayazidi 0.1%. Wasio na dini yoyote ni 41.9%.

Watu maarufu

Tazama pia

Marejeo

  1. "Dutch" kwa Kiingereza linamaanisha watu wa ng'ambo ya mfereji wa Kiingereza ambao tangu karne kadhaa huitwa "Waholanzi" au "watu wa Nchi za Chini" ("Nederland" - ing. Netherlands). Hadi miaka 400 iliyopita Uholanzi ilikuwa sehemu ya Milki ya Kijerumani na wenyewe mara nyingi walijiita kwa jina kama Wajerumani / Wadachi wengine yaani "Deutsch" au kwa lahaja ya huko "Duits" au kikamilifu zaidi "Nederduits" (Kidachi cha chini). Hii imehifadhiwa katika lugha ya Kiingereza. Tangu kujitenga na Ujerumani (rasmi mwaka 1648) watu wa Nchi za Chini waliacha polepole kujiita vile wakajiona ni tofauti na Wajerumani. Ila tu katika lugha ya Kiingereza jina lile la kale limehifadhiwa kwa sababu wanawaita Wajerumani kwa jina tofauti ("German", si "Deutsch - Duits - Dutch")
  2. The Latin name Sacrum Imperium (Holy Empire) is documented as far back as 1157. The Latin name Sacrum Romanum Imperium (Holy Roman Empire) was first documented in 1254. The full name "Holy Roman Empire of the German Nation" (Heiliges Römisches Reich Deutscher Nation, short HRR) dates back to the 15th century.
    Zippelius, Reinhold (2006) [1994]. Kleine deutsche Verfassungsgeschichte: vom frühen Mittelalter bis zur Gegenwart [Brief German Constitutional History: from the Early Middle Ages to the Present] (kwa German) (tol. la 7th). Beck. uk. 25. ISBN 978-3-406-47638-9.{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  3. Demshuk, Andrew (30 Aprili 2012). The Lost German East. ISBN 9781107020733. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Desemba 2016. {{cite book}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ujerumani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.