Piano
Piano (kutoka neno la Kiitalia linalofupisha jina asili "pianoforte") ni ala kubwa ya muziki yenye vibanzi (vinaitwa pia vipande au funguo) vyeupe na vyeusi ambavyo hubonyezwa na kutoa sauti tofauti. Sauti hutokea wakati nyundo ndogo zinapopiga nyaya zinazofungwa kwenye fremu ya metali.
Kinanda huwa na funguo 88 na kila mmoja una nyundo yake inayosogezwa kwa wenzo ndani ya piano na kupiga nyaya zenye unene na urefu tofauti ili zitoe sauti tofautitofauti.
Piano huwa pia na pedali mbili au tatu zinazokanyagwa kwa miguu. Kwa kutumia pedali, mpiga piano anaweza kubadilisha sauti kwa kusogeza kidogo nyundo inayogusa sehemu za nyaya tu na hivyo kubadilisha sauti. Pedali nyingine inamiliki vipande vya kitambaa vilivyokandamizwa juu ya nyaya na hivyo kufupisha au kurefusha muda wa kutolewa kwa sauti.
Vyombo vingine vinavyotumika pamoja na piano ni kama gitaa, ukulele, ngoma na kadhalika.
Ilhali piano halisi ni ala ya muziki nzito sana, inayohitaji watu 4-6 kuibeba, pia yenye bei kubwa inayohitaji masahihisho ya mara kwa mara ya nyaya zake, piano za kielektroniki ziligunduliwa zinazoiga sauti yake lakini ni nyepesi na zinapatikana kwa bei ndogo.
Kuna ala nyingine yenye msururu wa funguo wa kufanana, lakini sauti hazitolewi ka njia ya kupiga waya, ila kwa filimbi (Kinanda cha filimbi).
Picha
hariri-
Nyenzo zinazounganisha funguo na nyundo
-
Nyundo na nyaya
-
Sauti inasahihishwa kwa skrubu za kukazia au kulegeza nyaya
-
Nyaya za piano
-
Funguo hupigwa kwa vidole
-
Mfano wa sauti
-
Mfululizo wa sauti
-
Mpiga piano anacheza muziki wa Johann Sebastian Bach
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Piano kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |