Mwanakondoo wa Mungu
Mwanakondoo wa Mungu ni neno la Injili ya Yohane (1:29, 36) lililotamkwa na Yohane Mbatizaji kumhusu Yesu Kristo ili kumtambulisha kama kafara itakayotolewa kwa ukombozi wa binadamu wote: kwamba atabeba dhambi ya ulimwengu mzima na kuifidia kwa kujitoa kabisa.
Kwa Kilatini neno hilo ni Agnus Dei na linatumika kutajia mchoro wa mwanakondoo mwenye msalaba (au bendera ya msalaba) ukiwa ishara ya Kristo.
Agnus Dei ni pia jina la litania fupi ambayo inaanzia na maneno hayo na kutumika wakati wa Misa padri anapomega hostie takatifu na kuchanganya kipande na umbo la divai lililomo katika kikombe.
Litania fupi ya namna hiyo inapatikana pia katikati ya utenzi maarufu kwa jina la Kilatini "Gloria".
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwanakondoo wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |