1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaishambulia meli ya ngano kwenye Bahari nyeusi

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Urusi imeishambulia kwa kombora meli iliyokuwa inasafirisha ngano kuelekea Misri mapema leo katika Bahari Nyeusi. Kwa mujibu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky watu watatu wameuwawa kwenye tukio hilo.

https://p.dw.com/p/4kYrq
Nyambizi ya Urusi katika Bahari Nyeusi
Nyambizi ya Urusi katika Bahari NyeusiPicha: Sergei Malgavko/TASS/dpa/picture alliance

Zelensky kupitia ukurasa wake wa jukwaa la X amesema, meli hiyo ilishambuliwa muda mfupi baada ya kuondoka katika eneo la bahari la Ukraine. 

Katika hatua nyingine Urusi imedai kuwa imeikomboa sehemu kubwa ya Mkoa wake wa Kursk. Hayo ni kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Rais Zelenky wa Ukraine awali alikiri kuwa wanajeshi wa Moscow waliongeza kasi ya mashambulizi ya kulipa kisasi.

Soma pia:Urusi yashambulia kwa droni kaskazini mwa Ukraine

Itakumbukwa kuwa, Agosti 6, Kyiv ilifanya uvamizi wa kushtukiza ndani ya mkoa huo ulio  mpakani na Ukraine.