Waridi
Mandhari
Waridi ni maua mazuri sana ya mwaridi na walio wengi huvutiwa nayo sana kwa sababu ya rangi yao au hata harufu yao tu.
Bila shaka uzuri wa mwonekano wa maua haya huwafanya walio wengi kusahau kutazama namna ulivyo mmea wake. Ni ajabu sana ukiutazama mmea wa ua hili namna ulivyo. Kwanza umezungukwa na miiba pande zote ila cha ajabu ni kwamba kamwe miiba haichomani wala kugombana lakini pale ambapo mwanadamu anapoukaribia au kuuparamia bila umakini wowote ni lazima mwiba au miiba nayo imchome.
Ua hili hutumika sehemu nyingi duniani kama alama ya upendo.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waridi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |