Tungamo
Tungamo | |
---|---|
Alama za kawaida | |
Kizio cha SI | kilogramu |
Tungamo (pia: masi, kutoka Kiingereza: mass) katika elimu ya fizikia ni tabia ya maada, na kwa njia hii pia tabia ya gimba au dutu.
Kipimo sanifu cha kimataifa cha tungamo ni kilogramu. Alama yake katika fomula kwa kawaida ni .
Tungamo na uzito
[hariri | hariri chanzo]Tungamo ni tofauti na uzito lakini katika maisha ya kawaida hatuoni tofauti. Hivyo tunatumia kipimo cha kilogramu pia kwa kutaja uzito wa sukari tunayonunua. Lakini hali halisi uzito wa gimba au Tungamo ileile ni tofauti kutegemeana na uvutano mahali ilipo. Kwa mfano mtu akifika juu ya Mwezi uzito ni sehemu ya sita ya uzito wake duniani. Kwa hiyo mtu mwenye uzito wa kilogramu 60 duniani atakuwa na kilogramu 10 pekee akipimwa juu ya Mwezi. Sababu yake ni ya kwamba uvutano wa Mwezi ni ndogo kuliko duniani.
Tungamo na uvutano
[hariri | hariri chanzo]Uvutano wa gimba fulani unategemeana na tungamo yake. Kila kitu hata gimba dogo kama jiwe, meza au mtu lina uvutano wake. Ila tu tungamo kubwa ya Dunia yetu inafanya uvutano wake yaani nguvu inayosababisha ya kwamba watu na vitu havielei hewani bali kukaa kwenye uso wa ardhi tukivutwa kuelekea kitovu cha sayari yetu. Vitu vyote vinavyoshikwa na uvutano wa Dunia vina uvutano wao vilevile lakini kwa sababu tungamo ya watu na vitu ni ndogo kabisa kuliko tungamo ya Dunia hatuwezi kusikia tofauti. Pia Mwezi unavutwa na graviti ya Dunia yetu lakini tungamo ya Mwezi ni kubwa kiasi kwamba uvutano wa Mwezi unaathiri pia Dunia. Hii inaonekana kirahisi kutokana na mabadiliko ya bahari kuwa maji kujaa na kupwa yanayosababishwa na uvutano wa uvutano wa Mwezi.
Tungamo na inesha
[hariri | hariri chanzo]Tungamo inafanya pia inesha ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya tungamo kubaki katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje. Tungamo kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kwa urahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: tungamo zake ni tofauti, hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tungamo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |