Nenda kwa yaliyomo

Ngogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngogo
Ngogo macho-makubwa (Synodontis grandiops)
Ngogo macho-makubwa (Synodontis grandiops)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Siluriformes (Samaki kama kambale)
Familia: Mochokidae (Samaki walio na mnasaba na ngogo)
Jordan, 1923
Jenasi: Synodontis
G. Cuvier, 1816
Ngazi za chini

Spishi 131, 26 katika Afrika ya Mashariki:

Ngogo, gogo, kolokolo au ngonje ni samaki wa maji baridi wa jenasi Synodontis katika familia Mochokidae na oda Siluriformes ambao wanatokea Afrika tu. Jenasi hii ina spishi 131. Kwa Kiingereza huitwa squeakers kwa sababu wakati wanapokasirika au kutishwa wanatoa vilio vyembamba wakichua miiba pamoja.

Ngogo ni samaki wadogo hadi wakubwa kiasi na spishi nyingi zinaonyesha mabaka ya kuvutia. Wana paji la uso ngumu. Mapezi yanajumuisha pezimgongo na pezi lenye shahamu nyuma yake, mapeziubavu, mapezitumbo, pezimkundu na pezimkia. Tindi ya kwanza ya pezimgongo na mapeziubavu zimeshupazika kuwa miiba. Baadhi ya spishi hujulikana kwa tabia ya kiasili ya kuogelea tumbo juu, inayowapatia jina la ngogo juu-chini. Spishi nyingine, kajikijiki (Synodontis multipunctatus), ni kidusia wa kiota au ngogo-kekeo.

Ngogo ni samaki ya maji baridi ambao hupatikana katika Afrika nzima na kutokea hasa katika Afrika ya Kati na ya Magharibi. Ngogo ni jenasi ya Mochokidae iliyosambazwa zaidi na kutokea maji baridi mengi ya Afrika Kusini kwa Sahara na mfumo wa Mto Naili. Wanaweza kuishi katika maji baridi yanayoweza kuwa hori, mabwawa, maziwa, vijito na mito. Msambao wao ni sawa na ule wa chambo, lakini tofauti na chambo takriban bioanuwai yao yote hutokea katika mito badala ya maziwa.

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Synodontis hazikutopea na kula vyakula vingi mbalimbali. Wadudu, gegereka, moluska, anelidi, mbegu na miani imepatikana ndani ya tumbo ya spishi mbalimbali za ngogo. Wanajilisha kwa sakafu ya maji na huweza kuwa walatakataka, na spishi kadhaa zinaweza pia kujitohoa kwa kujilisha zikichuja maji. Hii inawawezesha kukabiliana na mabadiliko ya misimu na makazi na kuwapatia uwezo bora wa kuenea katika makazi tofauti. Spishi tofauti za ngogo zina kiwango cha ukuaji tofauti lakini wengi wao ni sawa. Majike ya spishi ni wakubwa kuliko madume kwa kawaida. Dume na jike wote wawili hukua haraka sana mwaka wa kwanza na kisha ukuaji hupungua huku wakizeeka. Umbo na muundo wa samaki hawa ni tofauti sana wakilinganishwa na samaki wengine. Ukubwa na umbo la kinywa ni tofauti kwa sababu kipo chini ya kichwa na kwa kawaida samaki hawa wana umbo la pembetatu au mcheduara wakiangaliwa kutoka upande. Hakuna vitu vingi vinavyojulikana kuhusu uzazi katika samaki hawa. Imegunduliwa kuwa Julai hadi Oktoba ni wakati wanapotaga na kwamba wanaogelea kwa jozi wakati huu. Wameonwa kutaga kwa kipindi cha mafuriko cha majira ya mvua.

Ngogo na watu

[hariri | hariri chanzo]

Spishi nyingi za ngogo ni samaki wa mapambo wanaopendezwa katika upendeleo wa ufugaji wa samaki. Wakati baadhi ya spishi zinathamini kwa sababu ya rangi au tabia zao, spishi nyingine zinahitajika kwa chakula. Spishi kubwa kadhaa za ngogo ni vyanzo muhimu vya chakula kwa watu wa Afrika.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.