Mmepulu
Mmepulu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mmepulu mkubwa kwenye Makumbusho ya Historia ya Asili, London
(Potamogale velox) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 2, spishi 3:
|
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wamepulu (kutoka Kiasoa: amepulu) au katewe (kutoka Kiluvale: katewe) ni wanyama wadogo wa familia Potamogalidae. Hawa ni wanyama wa maji ambao wanatokea misitu ya mvua ya Afrika kusini kwa Sahara. Wanafanana na fisi-maji wadogo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana mnasaba na tandaraka wa Madagaska. Wale wa jenasi Micropotamogale wana mwili wa sm 12–20 na mkia wa sm 10–15; wale wa Potamogale wana mwili wa sm 30–35 na mkia wa sm 25–29. Spishi zote zina manyoya mazito yenye rangi ya kijivu hadi kahawia lakini rangi ya chini ni takriban nyeupe. Hula wanyama wa maji kama gegereka, wadudu, konokono wa maji, samaki na vyura.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Micropotamogale lamottei, Mmepulu wa Mlima Nimba (Nimba Otter Shrew)
- Micropotamogale ruwenzorii, Mmepulu wa Ruwenzori (Ruwenzori Otter Shrew)
- Potamogale velox, Mmepulu Mkubwa (Giant Otter Shrew)
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.