Kipumbwi
Kipumbwi ni kata ya Wilaya ya Pangani katika Mkoa wa Tanga, Tanzania, yenye Postikodi namba 21311.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 12,268 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,876 waishio humo.
Kata hii ina vitongoji vinne ambavyo ni Serewani, Kipumwbwi Mtoni na Kipumbwi Mji Mpya.
Katika kata ya Kipumbwi, shughuli kubwa ya uchumi ni uvuvi. Wakazi wa Kipumbwi hujishughulisha na shughuli kadhaa za uzalishaji mali kama vile uvuvi, kilimo, biashara na usafirishaji.
Kipumbwi ni jina la kale kidogo kwenye pwani ya Uswahilini; wakati wa karne ya 19 Kipumbwi ilijulikana pale Mombasa kuwa mwisho wa eneo la Mrima[2].
5°38′S 38°54′E / 5.633°S 38.900°E
Marejeo
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Krapf aliandika katika kamusi yake: "MRIMA (ulio tini (chini) ya milima, ni Mrima, si kisiwa), a tract of country beginning with Oassi (Wasini) and stretching as far as the Pangani River and Kipumbui (Kipumbwi)"
Kata za Wilaya ya Pangani - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bushiri | Bweni | Kimang'a | Kipumbwi | Madanga | Masaika | Mikunguni | Mkalamo | Mkwaja | Mwera | Pangani Magharibi | Pangani Mashariki | Tungamaa | Ubangaa
|