Kaunti ya Tharaka-Nithi
Kaunti ya Tharaka-Nithi | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
| |||
Tharaka-Nithi County in Kenya.svg Kaunti ya Tharaka-Nithi katika Kenya | |||
Coordinates: 0°18′S 38°0′E / 0.300°S 38.000°E | |||
Nchi | Kenya | ||
Namba | 13 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki | ||
Makao Makuu | Kathwana | ||
Kikao cha Serikali | Chuka | ||
Gavana | Muthomi Njuki | ||
Naibu wa Gavana | Francis Nyamu Kagwima | ||
Seneta | Kithure Kindiki | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Beatrice Nkatha Nyaga | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Tharaka Nithi | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 15 | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 3 | ||
Eneo | km2 2 564.4 (sq mi 990.1) | ||
Idadi ya watu | 393,177 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 153 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | tharakanithi.go.ke |
Kaunti ya Tharaka-Nithi ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 393,177 katika eneo la km2 2,564.4, msongamano ukiwa hivyo wa watu 153 kwa kilometa mraba[1]..
Serikali huketi Chuka, ingawa makao makuu rasmi ni Kathwana.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Tharaka Nithi imepakana na kaunti za Meru, Embu, Kirinyaga, Nyeri na Kitui.
Ina sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya upande wa magharibi.
Mto Tana hupitia katika kaunti hii. Mito inayotiririsha maji ndani ya Mto Tana na hupitia Tharaka Nithi kutoka Mlima Kenya ni: Mto Mutonga, Mto Thingithu, Mto Kathita, Mto Thanantu, Mto Thangatha, Mto Kithinu na Mto Ura[2].
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Tharaka Nithi imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:
Eneo bunge | Kata |
---|---|
Maara | Mitheru, Muthambi, Mwimbi, Ganga, Chogoria |
Chuka/Igambango'mbe | Mariani, Karingani, Magumoni, Mugwe, Igambang’ombe |
Tharaka | Gatunga, Mukothima, Nkondi, Chiakariga, Marimanti |
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]
[hariri | hariri chanzo]- Igambang'ombe 53,210
- Maara 114,894
- Meru South 91,080
- Tharaka North 58,345
- Tharaka South 75,250
- Mt. Kenya Forest 398
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ "About - County Government of Tharaka Nithi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-04. Iliwekwa mnamo 2018-04-15.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Overview of Tharaka Nithi County Ilihifadhiwa 12 Februari 2019 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Tharaka-Nithi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |