Kasubi
Kasubi ni jina la kilima ndani ya mji wa Kampala mji mkuu wa Uganda. Kasubi imejulikana hasa kama mahali pa Makaburi ya Kasubi ya wafalme wa Buganda.
Mwaka 1882 ikulu ya Kabaka Mutesa I. ilijengwa kwenye kilima cha Kasubi. Alipokufa ikulu ikawa kaburi lake jinsi iliyvokuwa kawaida kati ya makabaka wa Buganda. Kuna desturi kwa makabila mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ya kuwa mtu atazikwa nyumbani kwake hakuna atakeyeikalia tena.
Kutokana na kuja kwa ukoloni hapakuwa tena na nafasi ya kumjengea kila Kabaka ikulu mpya hivyo Kasubi ikawa mahali pa kaburi wa makabaka waliomfuata Mutesa I. yaani Mwanga II., Daudi Chwa II. na Mutesa II..
Jengo kuu ni Muzibu Azaala Mpanga ambalo ni kuba kubwa lililojengwa kwa ubao na matete lenye ujuu wa 12 m na kipenyo cha 31m. Ujenzi huu ni namna ya kiutamaduni kwa ajili ya majengo ya kifalme katika Afrika ya Mashariki na Kati.
Majengo mengine hukaliwa na wanawake hasa wajane wa familia ya kifalme wenye wajibu wa kuyatunza makaburi.
Majengo yamo ndani ya eneo pana la hektari 30 ambalo sehemu kubwa hulimwa na wakina mama wanaotunza makaburi.
Kwa Waganda wengi makaburi ni kitovu cha kiroho. Tangu mwaka 2001 yameingizwa katika orodha la UNESCO la Urithi wa Dunia.
Mwaka 2010 jengo kuu lenye makaburi yenyewe lilichomwa motoni lililowaka kwa sababu zisizojulikana. Mabaki ya wafalme hayakuharibiwa. Kuna mipango ya kulijenga upya jinsi ilivyokuwa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 4 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
- Maelezo ya kamati ya UNESCO kuhusu makaburi ya Kasubi