Nenda kwa yaliyomo

Jane Goodall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jane Goodall

Jane Goodall (jina kamili: Valerie Jane Morris-Goodall; alizaliwa Hampstead, Uingereza, Aprili 1934) ni mwana anthropolojia na mwana primatolojia, maarufu kwa sababu aliandika na alifundisha watu wengi kuhusu sokwe.

Alisafiri katika nchi ya Tanzania, na aliishi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe ili kuona sokwe. Niliandika tasnifu yake ambaye inaitwa Behavior of Free-Living Chimpanzees.

Familia na Utoto

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake aliitwa Mortimer Herbert Morris-Goodall (1907-2001), na alikuwa mfanyabiashara. Mama yake aliitwa Margaret Mfanwe Joseph (1906-2000), na alikuwa mwandishi. Hakuwa na ndugu. Familia yake ilihama mpaka mji wa Bournemouth, na Jane Goodall alisoma hapa kwa shule ya msingi. Shule ya msingi inaitwa Uplands.

Safari yake ya Afrika Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
Sokwe

Jane Goodall alipenda wanyama, na hivyo aliamua kusafiri kwenda Afrika Mashariki mwaka wa 1957. Alienda Kenya ambapo alimtafuta rafiki yake Louis Leakey, mwanakiolojia aliyekuwa akiishi huko. Louis Leakey alimshauri Jane Goodall kusoma antropolojia katika chuo kikuu kabla ya kufanya kazi naye. Jane Goodall alisafiri kwenda Olduvai Gorge kukutana na Louis Leakey na Mary Leakey.https://education.nationalgeographic.org/resource/jane-goodall/%5D

Chuo Kikuu

[hariri | hariri chanzo]

Jane Goodall alisomea sayansi katika Chuo Kikuu cha Cambridge. Alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Newnham na Darwin pia. Hapo ndipo alipoandika tasnifu yake kwa mwalimu wake Robert Hinde. Alikuwa mwandishi wa kitabu chake cha kwanza, "Behavior of Free-Living Chimpanzees", kuhusu uchunguzi wake na uzoefu wake katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.

Hifadhi ya Tafia ya Gombe

Jane Goodall alifanya utafiti juu ya sokwe katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe mwaka wa 1960. Alikuwa na maoni kuwa sokwe wanaishi kama binadamu, na wanaweza kuwa na hisia kama za huzuni na hasira. Aliwatazama sokwe wakifanya vitendo vinavyofanana na vya binadamu, kama vile kubusu na kumbatiana. Pia alibaini kuwa sokwe hula nyama, jambo ambalo lilikuwa tofauti na imani ya awali kwamba wao hula majani tu. Jane Goodall alithibitisha pia kwamba sokwe ni wanyama wenye tabia za kihisia na wakali, ambao wanapenda kupigana.

Jane Goodall ameolewa mara mbili. Alikuwa na ndoa na Baron Hugo van Lawick mnamo Machi 28, 1964, huko London, na walikuwa na mtoto mmoja, Hugo Eric Louis. Baadaye, aliolewa na Derek Bryceson mnamo 1974, ambaye alikuwa mbunge katika Tanzania. Hata hivyo, alifariki kutokana na saratani.