Nenda kwa yaliyomo

Donna Auguste

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Donna Auguste (alizaliwa 1958) ni mfanyabiashara, mjasiriamali na mhisani wa mambo ya jamii wa Marekani mwenye asili ya Afrika.

Akishirikiana na mwenzake John Meier alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Freshwater Software kati ya mwaka 1996 mpaka 2000[1]. Kabla ya kuanzisha Freshwater, alikuwa mhandisi katika kampuni ya kompyuta ya Apple alikuwa anasaidia na kusimamia uundaji wa kifaa cha usaidizi wa kidigitali cha Newton[2].

Baada ya kuuza hisa zake za Freshwater Software kwa dolar miioni 147, Auguste alianzisha taasisi ya Leave a Little Room Foundation, LLC inayolenga kuwasaidia watu maskini wenye mahitaji kupata makazi, umeme na chanjo katika nchi mbalimbali.[3]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-16. Iliwekwa mnamo 2022-07-28.
  2. "She's Fresh - Black Enterprise". archive.ph. 2013-01-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-18. Iliwekwa mnamo 2022-07-28.
  3. https://www.informit.com/authors/bio/92bc70aa-1aec-43aa-8d9a-4f20fe7675d7 Donna Auguste, tovuti ya informit.com