Nenda kwa yaliyomo

Bara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
AmerikaUlayaAsiaAustraliaAustraliaAfrikaAntaktika
Ramani ya dunia inayoonyesha mabara
saba yanayohesabiwa kwa kawaida.

Bara (au kontinenti) ni pande kubwa la nchi kavu la Dunia linalozungukwa na bahari.[1] Kwa kawaida tunatofautisha mabara 7 ya Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antaktiki, Asia, Australia, na Ulaya.

Wazo la bara

Neno "bara" lamaanisha pande kubwa la nchi kavu , tofauti na bahari au visiwa vidogo karibu na pwani ya nchi kavu kubwa zaidi. Neno "kontinenti" latokana na Kilatini "terra continens" yaani "nchi (kavu) mfululizo".

Kwa hiyo elezo la neno bara / kontinenti katika sayansi ya jiografia ni "masi kubwa na mfululizo za nchi kavu zinazotengwa kwa maeneo makubwa ya maji"[2] Lakini hali halisi sehemu kubwa ya mabara saba yanayokubaliwa kwa kawaida hayatengwi kabisa kati yake kwa maji. Kwa mfano Ulaya na Asia hayatengwi kabisa na tofauti yake ni kihistoria na kiutamaduni, si kijiografia. Pia neno "masi kubwa" halieleweki waziwazi kabisa. Kwa nini Greenland yenye eneo la kilomita za mraba 2,166,086 inaitwa "kisiwa" lakini Australia yenye eneo la 7,617,930 huitwa bara?

Mabara yote ya Dunia yetu huwa na pwani kwenye bahari kuu ambayo ni moja tu ikigawiwa kwa sehemu mbalimbali na mabara vigezo vingine.[3][4]

Uenezaji wa bara

Kwa lugha ya kawaida “bara” ni eneo mfululizo wa nchi kavu. Kwa maana hii “Tanzania bara” ni eneo lote la Tanzania isipokuwa visiwa ambavyo ni sehemu ya nchi ya Tanzania bila visiwa vya Unguja, Pemba, Mafia na kadhalika.

Vivyo hivyo “Ulaya bara” ni eneo la Ulaya bila visiwa kama Britania, Eire, Malta na kadhalika.

Kwa macho ya jiolojia “bara” ni pana kuliko nchi kavu tu. Tunaangalia eneo lote la miamba inayounda bara. Siku hizi tunajua kwamba kila bara linalingana na kipande cha ganda la dunia tunachoita bamba la bara (continental plate). Kipande hiki kinaendelea pia chini ya uso wa bahari katika tako la bara (continental shelf) katika maji yasiyo na kina kikubwa pamoja na visiwa vya sehemu hizi. Kwa mtazamo huu visiwa vya Britania na Eire ni sehemu za Ulaya na vivyo hivyo Autralia na Guinea Mpya ni bara moja.

Kwa maana ya utamaduni wazo la bara linaweza kujumlisha pia visiwa vya mbali kama vile Iceland huhesabiwa sehemu ya Ulaya au hata mikoa ya Ufaransa katika Bahari Hindi kuhesabiwa kisiasa katika Ulaya.

Idadi ya mabara

Kwenye ramani zinazotumia lugha ya Kiingereza [5] kawaida huhesabiwa mabara saba duniani, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo.

  1. Bara la Afrika
  2. Bara la Asia
  3. Bara la Amerika ya Kaskazini
  4. Bara la Amerika ya Kusini
  5. Bara la Antaktika
  6. Bara la Ulaya
  7. Bara la Australia

Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlishwa pamoja na Australia kama

na kuhesabiwa kama bara.

Kutofautisha mabara

[[File:Continental models-Australia.gif|thumb|450px|Ramani inayoonyesha njia mbalimbali za kugawa dunia kwa mabara. Kutegemeana na mawazo ya wataalamu mabara huweza kuhesabiwa kwa namna tofauti. Kwa mfano Eurasia kwa kawaida huhesabiwa kuwa mabara 2 Ulaya na Asia (nyekundu). Wengine hujumlisha pia Eurasia pamoja na Afrika kuwa bara 1. Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini wakati mwingine hutazamiwa kuwa bara moja ya Amerika.

Kutokana na elezo kuu kuwa bara ni masi ya nchi kavu iliyotengwa na bara nyingine kwa maji kuna mawazo tofauti kuhusu idadi ya mabara.

  • Ulaya na Asia kwa pamoja ni masi moja kubwa ya nchi kavu na kijiografia hakuna tofauti. Sababu za kuzihesabu kuwa mabara mawili ni kiutamaduni na kihistoria tu. Kwa hiyo mara kwa mara kuna pendekezo kuzijumlisha kwa jina "Euroasia" au "Eurasia".
  • Afrika imeunganishwa na Asia kwa shingo ya nchi ya Suez.
  • Amerika Kusini na Amerika Kaskazini zinaunganishwa kwa shingo ya nchi ya Panama na hata hapo mara nyingi hujumlishwa kama "bara pacha"
  • Mfumo wa mabara saba hufundishwa kule China, India, Pakistan, Ufilipino, sehemu za Ulaya na katika nchi nyingi zinazotumia lugha ya Kiingereza pamoja na Australia[6] and England[7]
  • Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Eurasia bara moja) hutumiwa zaidi pale Urusi, Ulaya ya Mashariki na Japani
  • Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Amerika kuwa bara moja) hutumiwa Ufaransa na nchi zilizokuwa koloni zake na Italia, Urenol, Hispania, Romania, Amerika Kusini[8] Ugiriki,[9] na nchi kadhaa nyingine za Ulaya.
  • Kuna pia mfumo wa kuhesabu mabara matano kwa kuacha Antaktika isiyo wa wakazi kwenye msingi wa mabara sita. Huu unatumiwa katika nembo na katiba ya harakati ya Michezo ya Olimpiki.[10]
  • wataalamu wachache hupendelea mfumo wa mabara manne wakihesabu Afro-Eurasia bara moja

[11] wakibaki na Amerika, Afro-Eurasia, Australia na Antaktiki.

Mabara katika historia ya dunia

Picha ya dunia inyoonyesha jinsi gani bara ya kiasili ya Pangea iligawanyika

Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara linalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la Mabara ya Dunia

Bara Eneo (km²) Asilimia ya
nchi kavu yote
Wakazi
2008
Asilimia ya
Wakazi wa dunia
Msongamano
wa watu
kwa km²
Asia 43,820,000 29.5% 369,000,000 36% 86.70
Afrika 30,370,000 20.4% 222,011,000 22% 29.30
Amerika Kaskazini 24,490,000 16.5% 168,720,000 16% 21.0
Amerika Kusini 17,840,000 12.0% 152,000,000 15% 20.8
Antaktika 13,720,000 9.2% 1,000 0.00002% 0.00007
Ulaya 10,180,000 6.8% 203,000,000 20% 69.7
Australia 9,008,500 5.9% 32,000,000 0.3% 3.6

Eneo la dunia

Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu.

Jiolojia ya mabara

Mabara jinsi yanavyoonekana hukaa juu ya mabamba ya gandunia ambayo ni vipande vikubwa vya mwamba vinavyounda uso wa dunia. Mabara tunavyoyajua yanalingana kila moja na bamba lake na kila bamba ina mwendo wake wa polepole. Hii ni sababu ya kwamba baada ya miaka mingi uso wa dunia utaonekana tofauti kuliko leo.

Kijiolojia bara haliishi kwenye pwani pale bahari inapoanza. Bara linaendelea chini ya uso wa bahari kama tako la bara.

Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya.

Kwa jumla miamba ya sehemu za mabara ni mipesi kushinda miamba ya chini na hii ni sababu ziko juu ya miamba mingine.

Nchi za Mabara haya

  1. Bara la Asia lina nchi huru 44.
  2. Bara la Afrika lina nchi huru 53.
  3. Bara la Amerika ya kaskazini lina nchi huru 35.
  4. Bara la Antaktika halina wakazi wa kudumu wala nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili.
  5. Bara la Australia au Oshania lina nchi huru 14.
  6. Bara la Ulaya (au Uropa) lina nchi huru 46.

Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi.

Marejeo

  1. Ufafanuzi kufuatana na Kamusi Kuu ya Kiswahili, uk. 67; BAKITA 2015
  2. Lewis, Martin W.; Kären E. Wigen (1997). The Myth of Continents: a Critique of Metageography. Berkeley: University of California Press. uk. 21. ISBN 0-520-20742-4, ISBN 0-520-20743-2.
  3. "Ocean Ilihifadhiwa 26 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.". Columbia Encyclopedia (2006). New York: Columbia University Press. Retrieved 20 February 2007.
  4. "Distribution of land and water on the planet Ilihifadhiwa 31 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.." UN Atlas of the Oceans (2004). Retrieved 20 February 2007.
  5. pamoja na nchi zinazofuata mapokeo haya
  6. "F-10 Curriculum Geograph". Australian Curriculum, Assessment, and Reporting Authority. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-24. Iliwekwa mnamo 2016-04-02.
  7. "National curriculum in England: geography programmes of study". UK Department for Education.
  8. "Real Academia Española". Lema.rae.es. Iliwekwa mnamo 2013-09-30.
  9. [1] Older/previous official Greek Paedagogical Institute 6th grade Geography textbook (at the Wayback Machine), 5+1 continents combined-America model; Pankosmios Enyklopaidikos Atlas, CIL Hellas Publications, ISBN 84-407-0470-4, page 30, 5+1 combined-America continents model; Neos Eikonographemenos Geographikos Atlas, Siola-Alexiou, 6 continents combined-America model; Lexico tes Hellenikes Glossas, Papyros Publications, ISBN 978-960-6715-47-1, lemma continent (epeiros), 5 continents model; Lexico Triantaphyllide online dictionary , Greek Language Center (Kentro Hellenikes Glossas), lemma continent (epeiros), 6 continents combined-America model; Lexico tes Neas Hellenikes Glossas, G.Babiniotes, Kentro Lexikologias (Legicology Center) LTD Publications , ISBN 960-86190-1-7, lemma continent (epeiros), 6 continents combined-America model
  10. "Preamble" (PDF). Olympic Charter. International Olympic Committee. 8 Desemba 2014. uk. 10. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2015. the five interlaced rings, which represent the union of the five continents{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. R. W. McColl, ed. (2005). "continents". Encyclopedia of World Geography 1. Facts on File, Inc. p. 215. ISBN 9780816072293. Retrieved 2012-06-26. "And since Africa and Asia are connected at the Suez Peninsula, Europe, Africa, and Asia are sometimes combined as Afro-Eurasia or Eurafrasia."

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: