Kindi Mrukaji
Mandhari
(Elekezwa kutoka Anomaluridae)
Kindi mrukaji | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kindi mrukaji wa Pel (Anomalurus pelii)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3, spishi 7:
|
Kindi warukaji ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Anomaluridae. Wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Kuna kindi warukaji huko Asia pia, lakini jamii hizi hazina mnasaba. Wale wa Afrika wana ngozi kati ya miguu ya mbele na ya nyuma, isipokuwa spishi moja, kindi mkia-magamba. Upande wa chini wa msingo wa mkia wao mrefu una mistari miwili ya magamba yenye ncha kali yanayomsaidia mnyama ili kupanda juu ya miti. Rangi yao ni kijivu, kahawia, kahawiachekundu au hudhurungi. Hula matunda, makokwa, maua na majani na pengine wadudu pia.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Anomalurus beecrofti, Kindi Mrukaji wa Beecroft (Beecroft's Flying Squirrel)
- Anomalurus derbianus, Kindi Mrukaji wa Derby (Lord Derby's Scaly-tailed flying squirrel)
- Anomalurus pelii, Kindi Mrukaji wa Pel (Pel's Flying Squirrel)
- Anomalurus pusillus, Kindi Mrukaji Mdogo (Dwarf Scaly-tailed Squirrel)
- Idiurus macrotis, Kindi Mrukaji Masikio-marefu (Long-eared Flying Mouse)
- Idiurus zenkeri, Kindi Mrukaji Kibete (Pygmy Scaly-tailed Flying Squirrel)
- Zenkerella insignis, Kindi Mkia-magamba (Cameroon Scaly-tail)
Spishi ya kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Kabirmys qarunensis (Mwisho wa Eocene ya Birket Qarun, Misri)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kindi mrukaji wa Beecroft
-
Kindi mrukaji wa Derby
-
Kindi mrukaji mdogo
-
Kindi mrukaji kibete
-
Kindi mkia-magamba