Agata Kim Agi
Agata Kim Agi (alifariki Seoul, 24 Mei 1839) alikuwa mama wa familia aliyejiunga na Ukristo akabatizwa gerezani akisubiri kuuawa kwa ajili ya imani hiyo[1].
Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake kilichompata kwa kukatwa kichwa pamoja na Augustino Yi Kwanghon, Damiani Nam Myonghyok, Magdalena Kim Obi, Barbara Han A-gi, Ana Pak A-gi, Agatha Yi So-sa, Lusia Pak Hui-sun na Petro Kwon Tugin[3].
Mazingira
[hariri | hariri chanzo]Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/54610
- ↑ "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-06.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
- ↑ The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Attwater, Donald and Catherine Rachel John (1993). The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books. ISBN|0-14-051312-4.
- Dallet, Charles (1874). Histoire de l'Église de Corée, Volume 1. Paris: Librairie Victor Palmé.
- Dallet, Charles (1874). Histoire de l'Église de Corée, Volume 2. Paris: Librairie Victor Palmé.
- Fathers of the London Oratory (1859). The New Glories of the Catholic Church. London: Richardson and Son.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Homily of Pope John Paul II given for the Mass for the canonization of the Korean martyrs
- List and brief description of martyrs
- History of the Missions Etrangeres de Paris MEP
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |