Mtume Bartolomayo
Mitume wa Yesu |
---|
|
Bartolomayo (kwa Kigiriki Βαρθολομαιος) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu kadiri ya Injili Ndugu.
Wengi wanaona hilo ni ubini wake (kwa Kiaramu lina maana ya "mwana wa Tolomayo"), kumbe jina lake mwenyewe ni "Natanaeli", kama anavyotajwa na Injili ya Yohane 1:45, rafiki wa Mtume Filipo. Kama ni hivi, alikuwa mwenyeji wa Kana ya Galilaya, na unyofu wake ulisifiwa na Yesu mara alipokutana naye kwenye mto Yordani.
Anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 24 Agosti[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Yote tunayoyajua kwa hakika juu yake yanategemea Injili na Matendo ya Mitume anapotajwa tu katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama mwanzo mpya wa taifa la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.
Baada ya ufufuko wa Yesu na Pentekoste, hakuna habari za hakika, ila kuna masimulizi ya utume wake Mashariki ya Kati hadi India[2].
Alifia dini ya Ukristo katika nusu ya pili ya karne I labda Syria au Armenia kama si India.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kifodini cha Mt. Bartolomayo, Milano, Kanisa la Mt Bartolomayo
-
Giovan Battista Piazzetta, Kifodini cha Mt. Bartolomayo, 1722, Venezia, Kanisa la Mt. Stae
-
Sanamu ya Mt. Bartolomayo katika Kanisa kuu la Milano
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kwa Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Kwa lugha nyingine
[hariri | hariri chanzo]- Easton's Bible Dictionary, 1897.
- Encyclopedia Anglicana, 1911
- Dictionary of First Names, Patrick Hanks and Flavia Hodges. Oxford University Press, 1996
- Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
- The Apostles In India by Fr A.C Perumalil SJ 1952
- For a discussion of Baroque paintings of St. Bartholomew by the Spanish artist Ribera, see: Williamson, Mark A. "The Martyrdom Paintings of Jusepe de Ribera: Catharsis and Transformation", PhD Dissertation, Binghamton University, Binghamton, New York 2000 (available online at myspace.com/markwilliamson13732)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Life, Miracles and Martyrdom of St Bartholomew the Apostle of Jesus Christ Ilihifadhiwa 12 Agosti 2014 kwenye Wayback Machine.
- The Martyrdom of the Holy and Glorious Apostle Bartholomew, attributed to Pseudo-Abdias, one of the minor Church Fathers
- St. Bartholomew's mission in India
- St. Bartholomew's Connections in India
- "St. Bartholomew". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- St. Bartholomew page at Christian Iconography
- "The Life of St. Bartholomew the Apostle" Ilihifadhiwa 7 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine. in the Caxton translation of the Golden Legend
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Bartolomayo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |