Nenda kwa yaliyomo

Kiesperanto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Kiesperanto

Kiesperanto ni lugha ya kupangwa inayozungumzwa zaidi. Ilipangwa na L.L.Zamenhof, myahudi aliyetoka mjini Białystok, nchini Urusi (siku hizi ni sehemu ya nchi ya Poland). Alitoa kitabu cha kwanza cha lugha hii mwaka 1887 baada ya kuitengeneza kwa miaka karibu kumi. Nia yake ilikuwa kutengeneza lugha rahisi ili iwe lugha saidizi ya kimataifa, lugha ya pili kwa kila mtu duniani. Waesperanto wengine bado wanataka hiyo, lakini wengine wanapenda kuitumia tu bila nia ya kuieneza duniani kote.

Waesperanto wanakitumia Kiesperanto kwa ajili ya kukutana na wageni na kujifunza kuhusu nchi na tamaduni nyingine. Siku hizi, maelfu ya watu wanaitumia mara kwa mara ili kuwasiliana na watu popote duniani.

Chunguzi za kitaalamu zimeonyesha kwamba Kiesperanto kinaweza kujifunzwa rahisi zaidi sana kuliko lugha asilia, na pia kwamba kujifunza Kiesperanto kwanza kunarahisisha kujifunza kwa lugha nyingine.

Viungo vya nje