Nenda kwa yaliyomo

Baraza la Kiswahili la Taifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 00:41, 30 Oktoba 2006 na Marcos (majadiliano | michango)

BAKITA ni kifupi chake cha Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania. BAKITA ni chombo cha serikali chini ya wizara ya Habari Utamaduni na Michezo. Baraza liliundwa na sheria ya bunge Na. 27 ya mwaka 1967 kwa shabaha ya kukuza,kuimarisha na kuendeleza Kiswahili hasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanyika mwaka 1983 kwa Sheria ya Bunge Na. 7, BAKITA limepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili katika nchi za nje pia.

Pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) cha Kenya na wawakilishi kutoka Uganda BAKITA imeunda Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA).

Viungo vya Nje

Habari za serikali kuhusu BAKITA

MRADI WA KUSWAHILISHA PROGRAMU HURIA - Utangulizi unaeleza historia ya BAKITA (PDF)

en: "Govt appoints new BAKITA members" (taarifa ya "Guardian" ya Dar es Salaam Septemba 2006