Nenda kwa yaliyomo

Melanesia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 12:12, 8 Desemba 2020 na Olimasy (majadiliano | michango) (marekebisho ya kisarufi)
Mahali pa Melanesia katika Pasifiki kaskazini ya Australia
Mwenyeji wa Vanuatu awafundisha watoto kutengeneza moto

Melanesia ni eneo la Bahari ya Pasifiki kaskazini mwa Australia. Ni moja kati ya makundi makubwa matatu ya visiwa vya Pasifiki pamoja na Mikronesia na Polynesia.

Jina lake limeundwa na maneno ya Kigiriki ya μέλας cheusi na νῆσος kisiwa yaani "visiwa vyeusi" au zaidi "Visiwa vya Weusi". Nahodha Mfaransa Jules Dumont d'Urville alitunga jina hili mwaka 1832 akitaka kutaja wakazi wazalendo waliokuwa na rangi nyeusi-nyeusi.

Watu na utamaduni

D'Urville alijumlisha wakazi wa visiwa hivi pamoja kutokana na rangi yao. Lakini hali halisi ni watu wa aina mbalimbali. Wengine ni Waaustronesia, wengine Wapapua na wengine watu kutokana na mchanganyiko wa vikundi hivi viwili.

Nchi za Melanesia

Fiji, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon, Vanuatu na Kaledonia Mpya (chini ya Ufaransa) zinajihesabu kuwa sehemu za Melanesia. Kuhusu visiwa vingine mawazo hutofautiana.

Visiwa vya Melanesia

Visiwa na funguvisiwa zifuatazo zinahesabiwa katika Melanesia:

Visiwa vilivyoko katika eneo hili lakini wakazi hawajitazami kuwa Wamelanesia:

Wakati mwingine hata visiwa upande wa Guinea Mpya vinahesabiwa humo ingawa wakazi hawajitazami hivyo: Halmahera, Alor na Pantar.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.