Nenda kwa yaliyomo

Venezuela : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: eml:Venesüela
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: am:ቬኔዝዌላ
Mstari 171: Mstari 171:
[[af:Venezuela]]
[[af:Venezuela]]
[[als:Venezuela]]
[[als:Venezuela]]
[[am:ቬኔዝዌላ]]
[[an:Venezuela]]
[[an:Venezuela]]
[[ang:Feneswela]]
[[ang:Feneswela]]

Pitio la 18:52, 24 Septemba 2011

República Bolivariana de Venezuela1
Jamhuri ya Kibolivar ya Venezuela1
Bendera ya Venezuela Nembo ya Venezuela
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: None 2
Wimbo wa taifa: Gloria al Bravo Pueblo
Lokeshen ya Venezuela
Mji mkuu Caracas
10°30′ N 66°58′ W
Mji mkubwa nchini Caracas
Lugha rasmi Kihispania 3
Serikali Shirikisho la jamhuri
Hugo Chávez Frías
Uhuru
Kutoka Hispania
Kutoka Gran Colombia
ilitambuliwa

5 Julai 1811
21 Novemba 1831
30 Machi 1845
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
916,445 km² (ya 33)
0.3
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
26,749,000 (ya 43)
23,054,210
29/km² (ya 175)
Fedha Bolivar (VEB)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
AST (UTC-4:30)
None (UTC)
Intaneti TLD .ve
Kodi ya simu +58

-

1 Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela imekuwa jina la nchi tangu katiba ya 1999. "Kibolivar" ni jina la heshima kwa kumbukumbu ya mshujaa wa uhuru Simon Bolivar.
2 Zamani: Dios y Federación ("Mungu na Shirikisho")
3 Katiba inatambua pia lugha asilia zote nchini.


Ramani ya Venezuela

Venezuela ni nchi katika Kaskazini ya Amerika ya Kusini. Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.

Mbele ya pwani la nchi katika Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.

Venezuela ilikuwa koloni ya Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.

Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri na mji mkuu wa kitaifa ni Caracas.

Asili ya jina "Venezuela"

Jina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania Amerigo Vespucci aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katika maji karibu na mwambao pasipo na kina. Vijiji vilimkubusha juu ya mji wa Venezia uliojengwa vile. Venezuela yamaanisha "Venezia Ndogo" katika Kihispania.

Jiografia

Faili:Palafito Venezuela.PNG
Nyumba ya "palafito" jinsi ilivyoonekana zamani za Amerigo Vespucci

Venezuela ina eneo la 916,445 km² (kama Namibia) ikiwa na pwani lenye urefu la 2,800 km. Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kulimwa 4%, eneo la mifugo 20%, mazao ya kudumu kama kahawa 1%.

Kuna kanda nne za kijiografia:

  • tambarare za pwani karibu na Maracaibo katika kaskazini-magharibi
  • milima ya Andes
  • tambarere za mto Orinoko katikati ya nchi
  • nyanda za juu za Guayana katika kusini-mashariki

Milima ya meza

Nyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee kuna milima ya meza 115 inayoitwa "tepui" katika lugha ya wenyeji asilia. Kiekolojia hii ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama za pekee tofauti na milima jirani inayopatikana hapa tu kote duniani.

Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko Salto del Angel ("anguko la malaika") ambako maji huanguka mita 965.

Mito

Mto mkubwa wa Venezuela ni Orinoco mwenye urefu wa 2574 km unaoishia katika Atlantiki. Lakini mkono wa Brazo Casiquiare unajitenga na kuishia katika mto wa Amazonas nchini Brazil.

Tawimito muhimu ya Orinoco ni Rio Apure na Rio Caroni.

Majimbo katika shirikisho

Tazama pia Majimbo ya Venezuela
Mlima wa meza Mt. Roraima
Los Barrios ni mitaa ya vibanda vya Caracas
Faili:Caracas-downtown.jpg
Caracas ya kisasa

Venezuela ni shirikisho la madola au majimbo 23 ya kujitawala, maeneo yasiyojitawala na mkoa wa shirikisho la Caracas.

Jimbo Mji Mkuu Wakazi Eneo Kanda
Amazonas Puerto Ayacucho 70,464 180,144 km² Guayana
Anzoátegui Barcelona 1,222,225 43,300 km² Nor - Oriental
Apure San Fernando de Apure 377,756 76,500 km² Llanos
Aragua Maracay 1,449,616 7,014 km² Central
Barinas Barinas 624,508 35,200 km² Andean
Bolívar Ciudad Bolívar 1,214,846 238.000 km² Guayana
Carabobo Valencia 1,932,168 4,650 km² Central
Cojedes San Carlos 253,105 14,800 km² Central
Delta Amacuro Tucupita 97,987 40,200 km² Guayana
Falcón Coro 763,180 24,800 km² Central - Occidental
Guárico San Juan de los Morros 627,086 64,986 km² Llanos
Lara Barquisimeto 1,556,415 19,800 km² Central - Occidental
Mérida Mérida 715,268 11,300 km² Andean
Miranda Los Teques 2,330,872 7,950 km² Capital
Monagas Maturín 712,626 28,930 km² Nor - Oriental
Nueva Esparta La Asunción 712,626 1,150 km² Insular
Portuguesa Guanare 725,740 15,200 km² Central - Occidental
Sucre Cumaná 786,483 11,800 km² Nor - Oriental
Táchira San Cristóbal 992,669 11,100 km² South - Occidental
Trujillo Trujillo 608,563 7,400 km² Andean
Vargas La Guaira 298,109 1,496 km² Capital
Yaracuy San Felipe 499,049 7,100 km² Central - Occidental
Zulia Maracaibo 2,983,679 63,100 km² Zulian
Dependencias Federales (maneo chini ya shirikisho) - 2,245 342 km² Insular (visiwa)
Distrito Federal Caracas (Mkoa wa shirikisho) - 2,284,921 433 km² Capital (mji mkuu)

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Venezuela kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.