Amina
Wikipedia:Babel | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
|
Nimekuta hao watu wanaoamini kuwa Kiswahili hakifai kutumika katika sayansi, hasa katika elimu ya juu. Wanaamini kuwa lugha ya Kiingereza pekee ndyio kinafaa kuwa lugha ya mafundisho. Dhidi ya maoni hayo ninaamini kuwa lugha zote zinafaa, na Kiswahili ni lugha nzuri pia. Nimeunga mikono yangu katika Wikipedia ili kupandisha na kupanusha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mtandao na elimu.
Mambo zaidi ya hayo, jina ninalotumia kwenye Wikipedia ni jina ambalo nalipenda sana. Ni mtu wa kuzaliwa hapa Ulayani kwa hiyo siyo Mswahili kama wasomaji wengi wa Wikipedia wanavyofikiri.
Nilianza kujifunza Kiswahili baada ya kukutana na Watanzania wachache wa hapa na kujiunganisha katika chama kinachoshugulishia maendeleo ya maisha katika wilaya fulani wa mkoa wa Singida, nchini Tanzania. Baada ya hapo nikawa na nafasi ya kwenda kutembelea Tanzania na kuangalia maisha yakoje. Nimendelea kujiendeleza na kujifunza Kiswahili baadaye.