Mfumo wa chama kimoja
Mfumo wa chama kimoja ni utaratibu wa kisiasa unaoruhusu chama cha kisiasa kimoja tu.
Mara nyingi mfumo huo umeanzishwa kwa kupiga marufuku vyama vyote vingine. Kuna pia nchi ambako vyama mbalimbali viko, lakini havina nafasi ya kushiriki katika uchaguzi au vinazuiwa kushindana na chama tawala.
Kihistoria mifumo hii ilitokea katika mazingira ya Ukomunisti, Ujamaa au Ufashisti. Mfumo huu ni karibu na udikteta.
Mfumo wa chama kimoja katika Afrika
Afrika ilikuwa na kipindi kirefu cha utawala wa chama kimoja baada ya mwisho wa ukoloni. Nchi nyingi zilizorithi katiba za vyama vingi vilibadilisha katiba na kuwa na mfumo wa chama kimoja.
Sababu yake ilikuwa hasa ya kwamba vyama vya kisiasa vilikuwa vya kikabila, si ya kitaifa. Athira ya mfano wa Umoja wa Kisovyeti na China ilikuwa muhimu pia.
Tangu miaka ya 1990 ilionekana ya kwamba kwa jumla nchi zilizofuata mfumo huu zilibaki nyuma na karibu nchi zote za Afrika - isipokuwa Eritrea - ziliruhusu tena vyama vya upinzani angalau kwa jina.
Nchi za Afrika ya Mashariki zilizokuwa na mfumo wa chama kimoja
- Ethiopia (Chama cha Wafanyakazi cha Ethiopia) 1987-1991
- Kenya (Kenya African National Union) 1982-1990
- Malawi (Malawi Congress Party) 1966-1993
- Somalia (Chama cha kimapinduzi ya kijamii ya Kisomali) 1976-1991
- Tanzania (Tanganyika African National Union) 1965-1975; Zanzibar (Afro-Shirazi Party 1965-1992; TANU na ASP zikaungana kuwa (Chama Cha Mapinduzi) 1975-1992
- Uganda (National Resistance Movement/Party) 1987-2005
- Zambia (United National Independence Party) 1972-1990
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |