Mgawanyo wa madaraka

Pitio kulingana na tarehe 03:12, 7 Februari 2010 na Xqbot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: be:Падзяленне ўлады; cosmetic changes)

Mgawanyo wa madaraka ni mafundisho ya kisiasa yanayotofautisha kati ya mikono au mihimili 3 ya mamlaka katika dola.

Mihimili mitatu ni:

  • bunge au mamlaka ya kutunga sheria
  • serikali au mamlaka ya utendaji inayotekeleza sheria
  • mahakama au mamlaka ya kuamulia sheria

Falsafa ya mgawanyo wa madaraka

Hoja la kimsingi ni kugawanya madaraka kati ya mikono mbalimbali inayotakiwa kuatazamiana, kurekebishana na kusaidiana.

Wafuasi wa fundisho hili huona ya kwamba haki za watu huwa salama katika mfumo huu kuliko penye mamalaka yote katika mkono mmoja kama jinsi ilivyo katika hali ya udikteta.

Serikali inatawala kwa kutumia sheria lakini haiwezi kutunga sheria peke yake zitakazoongeza mamlaka yake mno.

Bunge inatunga sheria lakini haiwezi kufaidika na utekelezaji yake moja kwa moja.

Mahakama inaangalia sheria na kuamua juu ya matumizi yake. Inatakiwa kuzuia serikali inapoenda nje ya sheria.

Historia

Mgawanyo wa madaraka si jambo jipya katika historia.

Jamii kadhaa za Afrika zilipakana mamlaka ya chifu kwa kumpa sharti ya kuelewana na washauri au baraza la wazee kwa mipango muhimu.

Waroma wa Kale waligawa madaraka ya jamhuri kati ya seneti, mikutano ya raia wa kawaida na maafisa wa utendaji waliochaguliwa kwa muda.

Fundisho la kisasa lilitungwa na Mfaransa Charles-Louis Montesquieu katika kitabu chake "De l'ésprit des lois" (roho ya sheria) mwaka 1748.

Marekani na Ufaransa zilikuwa nchi za kwanza zilizoingiza mfumo huu katika katiba zao.

Siku hizi ni nchi nyingi duniani zinazofuata mfumo huu.