Nenda kwa yaliyomo

Shimo jeusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Shimo nyeusi)
Uchoraji wa shimo jeusi jinsi wataalamu wanavyoliwaza kabla ya mwaka 2019 ambapo hakukuwa na picha halisi ya shimo jeusi.
Picha ya shimo jeusi kwenye kitovu cha galaksi Messier 87 (picha iliyounganishwa kutoka vipimo vingi).

Shimo jeusi (kwa Kiingereza: black hole) ni jina la eneo katika anga-nje lenye mvutano kubwa, kiasi kwamba hata nuru haiwezi kutoka nje yake. Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huo ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na mvutano wa shimo jeusi. Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofikia upeo huo inamezwa kabisa, hakuna inayorudishwa tena.

Hadi sasa haijawezekana kutazama shimo jeusi moja kwa moja. Lakini wataalamu wa fizikia waliwahi kuyatabiri mashimo hayo. Hasa nadharia ya uhusianifu ilitabiri ya kwamba gimba lenye masi kubwa iliyokandamizwa katika eneo dogo litasababisha "shimo jeusi".

Katika miaka ya nyuma wataalamu wa anga wameangalia mahali pengi ambako mwendo wa nyota za eneo fulani si kawaida: unaelezwa kwa kuwepo kwa shimo jeusi katika sehemu hizo maana yake mvutano wake unaathiri mwendo wa nyota au mawingu ya gesi ya angani na kuzivutia kwake. Mwendo huu wa magimba katika mazingira ya mashimo meusi unaonekana kwa wataalamu wa anga.

Mnamo Machi 2019 wataalamu wa anga walifaulu kupata picha kwa kuunganisha vipimo vya paoneaanga kadhaa duniani kote vilivyolengwa vyote majarra Messier 87 (pia: Virgo A) na kupima kama darubini moja kubwa[1]. Mnamo Machi 2021 walifaulu kutoa picha mpya inayowezesha kuelewa zaidi kinachosababisha nusuranyota.

Inaaminiwa kwamba mashimo meusi hutokea wakati wa kufa kwa nyota kubwa zenye masi inayozidi masi ya Jua letu mara tatu au zaidi. Hutokea pia katika viini vya majarra penye maada nyingi kwa karibu.

Marejeo

  1. First M87 Event Horizon Telescope Results. I. The Shadow of the Supermassive Black Hole, tovuti ya iopscience, jarida la Institute of Physics (IOP) ambayo ni shirika la wanafizikia wa Uingereza na kimataifa

Viungo vya nje

Videos
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shimo jeusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.