Nenda kwa yaliyomo

YouTube

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waanzilishi wa YouTube. kulia ni Chad Hurley, Steve Chen na kushoto ni Jawed Karim

YouTube ni tovuti ya kushirikisha video ambazo watumiaji wanaweza kuzinakili na kuzigawa kwa wengine. Wafanyakazi watatu wa zamani wa PayPal waliunda YouTube mnamo Februari 2005. [1]

Mnamo Novemba 2006, YouTube, LLC ilununuliwa na Google Inc kwa Dola bilioni 1.65, na sasa huendeshwa kama shirika dogo la Google. Kampuni hii ipo San Bruno, California na inatumia teknolojia ya Adobe Flash kuonyesha aina mbalimbali za video zilizotengenezwa na watumiaji, pamoja na vijisehemu vya sinema, vijisehemu vya maonyesho ya runinga, na video za nyimbo, vilevile maudhui ambayo hayajakomaa kama vile video za kublogu na video za asili zilizo fupi.

Ikoni kamili ya rangi ya YouTube

Maudhui mengi yaliyomo kwenye YouTube yametumiwa na watu binafsi, ingawa vyombo vya habari pamoja na makampuni yakiwemo CBS, BBC, UMG na mashirika mengine hutoa baadhi ya habari zao, kama sehemu ya mpango wa ushirikiano na YouTube. [2]

Watumiaji ambao hawajasajiliwa wanaweza kutazama video, wakati watumiaji waliosajiliwa wanaruhusiwa kutumia na kunakili idadi isiyo na kipimo ya video. Video ambazo zanaweza kuwa na maudhui yaliyo na ujumbe wenye lugha isiyoruhusiwa zinapatikana kwa watumiaji waliosajiliwa tu na wenye umri zaidi ya miaka 18. Kunakili kwa video zenye lugha ya kukashifu, mambo ya ngono, ukiukwaji wa hakimiliki, na habari zinazohimiza uhalifu kumepigwa marufuku katika mkataba wa masharti ya huduma ya YouTube.

Akaunti za watumiaji waliosajiliwa hujulikana kama "channels". [3]

Historia ya kampuni

Makao makuu ya sasa ya YouTube mjini San Bruno, California.

YouTube ilianzishwa na Chad Hurley, Steve Chen na Jawed Karim ambao awali wote walikuwa wafanyakazi wa PayPal. [4] Hurley alisomea urasimu katika Chuo Kikuu cha Indiana ya Pennsylvania, huku Chen na Karim wakisomea kompyuta sayansi pamoja katika Chuo Kikuu cha Illinois huko Urbana-Champaign.[5]

Kulingana na hadithi inayorudiwa mara nyingi katika vyombo vya habari, Chad Hurley na Steve Chen waliibua wazo la YouTube wakati wa miezi ya mwanzo ya 2005, baada ya kukabiliana na matatizo ya kugawa video zilizochukuliwa kweye chakula cha jioni nyumbani kwa Chen huko San Francisco. Jawed Karim hakuhudhuria sherehe hii na alikana kwamba sherehe ilikuwepo, na Chad Hurley alisema kuwa, wazo kuwa YouTube lilianzishwa baada ya chakula cha jioni" pengine lilitiwa nguvu sana na mawazo ya matangazo ili kuunda hadithi yenye kueleweka zaidi." [6]

YouTube ilianza kama teknolojia ya kufadhiliwa, hasa kutoka kwa uwekezaji wa dola za Marekani milioni 11.5 kutoka kwa Sequoia Capital kati ya Novemba 2005 na Aprili 2006. [7] Hapo awali makao makuu ya YouTube yalikuwa upande wa juu wa Pizzeria na mkahawa wa Kijapani katika San Mateo, California. [8] Jina la kikoa chake www.youtube.com kilianza kutumika tarehe 15 Februari 2005, na tovuti iliundwa miezi kadhaa iliyofuata. [9] Video ya kwanza kwenye Youtube ilikuwa Me at the Zoo, na mwanzilishi wa onyesho Jawed Karim kwenye San Diego Zoo. [10] Video hii ilipakiwa mnamo tarehe 23 Aprili 2005, na bado yaweza kutazamwa kwenye tovuti. [11]

YouTube iliupatia umma toleo la kwanza la tovuti Mei 2005, miezi sita kabla ya uzinduzi rasmi mnamo Novemba 2005. Tovuti ilikua haraka, na Julai 2006 kampuni ilitangaza kwamba zaidi ya video mpya 65,000 zilikuwa zikipakiwa kila siku, na kwamba tovuti ilikuwa ikipokea watazamaji wa video milioni 100 kwa siku. [12] Kulingana na tarakimu zilizochapishwa na kampuni ya utafiti wa masoko comScore, YouTube inaongoza katika utoaji wa video kwenye mtandao katika Marekani, ikiwa na mgawo wa soko wa karibu asilimia 43 na zaidi ya video bilioni sita zilizotazamwa mnamo Januari 2009. [13] Inakadiriwa kuwa video mpya za jumla ya masaa 20 hupakiwa kwa tovuti kila dakika, na kwamba karibu robo tatu ya nyenzo hizi hutoka nje ya Marekani. [14] [15] Pia inakadiriwa kwamba katika mwaka 2007 YouTube ilitumiwa kipimo data sawa na kiasi kilichotumika kwenye wavuti mzima wa mwaka 2000. [16] Mwezi Machi 2008, kipimo data cha YouTube kiligharimu dola milioni 1 za Marekani kwa siku. [17] Alexa ameipa nafasi ya nne YouTube kama tovuti iliyotumiwa kwa wingi kwenye wavuti, nyuma ya Google, Yahoo! na Facebook.[18]

Uchaguzi wa jina www.youtube.com ulisababisha matatizo kwa vile jina hili lilikuwa likitumika kwa tovuti, www.utube.com. Mmiliki wa tovuti, Universal Tube & Rollform Equipment, aliandikisha kesi mahakamani dhidi YouTube Novemba 2006 baada ya kupokea idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitafuta YouTube. Universal Tube kwa sasa imebadilisha jina la tovuti yake na kuwa www.utubeonline.com. [19] [20]

Mnamo Oktoba 2006, Google Inc ilitangaza kwamba ilikuwa imeipata YouTube kwa dola bilioni 1.65 katika hisa za Google, agano hili lilikamilishwa tarehe 13 Novemba 2006. Google huwa haitoi tarakimu za kina za gharama ya kutunza YouTube, na mapato ya YouTube ya mwaka 2007 yalibainishwa kuwa "siyo kitu" katika uwekaji jalada. Juni 2008 nakala katika gazeti la Forbes lilitoa makadirio ya mapato ya 2008 kuwa dola milioni 200 za Kimarekani, huku likibaini mafanikio katika mauzo ya matangazo.

Mnamo Novemba 2008, YouTube ilifikia makubaliano na MGM, Lions Gate Entertainment na CBS ambazo ziliruhusu makampuni kutuma filamu nzima na maonyesho ya televisheni kwenye tovuti, yakiandamana na matangazo. Hatua hii imekusudiwa kutoa ushindani kwa tovuti kama Hulu, ambazo huwa na nyenzo kutoka kwa NBC, Fox, na Disney. [21] [22]

Tarehe 9 Oktoba 2009, wakati wa ukumbusho wa tatu kutoka kuchukuliwa na Google, Chad Hurley alitangaza katika chapisho la blogu ya kwamba YouTube ilikuwa inatumiwa na "zaidi ya watazamaji bilioni moja" duniani kote.

Athari za kijamii

Kabla ya uzinduzi wa YouTube mwaka 2005, kulikuwa na mbinu chache rahisi zilizokuwemo kwa watumiaji wa kompyuta wa kawaida ambao walitaka kuchapisha video kwenye wavuti. Pamoja na kusano lake rahisi, YouTube ilirahisisha uwezekano wa mtu yeyote aliyeunganishwa kwa wavuti kuchapisha video ambazo watazamaji duniani kote wanaweza kutazama kwa muda wa dakika chache. Mada tofauti zilizoko katika YouTube zimegeuza ugawi wa video kuwa mojawapo ya sehemu muhimu ya utamaduni wa wavuti.

Mfano wa awali wa athari za kijamii za YouTube ulikuwa ufanisi wa video ya Bus Uncle mwaka 2006. Inaonyesha mazungumzo makali kati ya kijana na mzee ndani ya gari la abiria huko Hong Kong, na ilijadiliwa sana katika wasimamizi wa vyombo vya habari vilivyoimarika. [23] Video nyingine iliyopokea uwambo ni guitar, [24] ambayo ilihusisha uiigizi wa Pachelbel's Canon huku akiwa na gitaa la umeme. Jina la mwigizaji halijatolewa katika video, na baada ya kupokea mamilioni ya maoni gazeti la The New York Times lilifichua jina la mcheza gitaa kama Jeong-hyun Lim, wa umri wa miaka 23 kutoka Korea ya Kusini ambaye alikuwa amerekodi traki hii ndani ya chumba chake cha malazi. [25]

YouTube ilipatiwa tuzo la 2008 la George Foster Peabody na kunukuliwa kuwa " 'Uwanda wa Wasemi' " na iliyoonyesha na kukuza demokrasia." [26] [27]

Lawama

Nyenzo zenye hakimiliki

YouTube imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuhakikisha kwamba video zake zina heshimu sheria ya hakimiliki. Wakati wa kupakia video,watumiaji wa YouTube huwa wanaonyesha daima kiwambo chenye ujumbe ufuatao:

Usipakie maonyesho yoyote ya televisheni, video za nyimbo, tamasha za miziki au ujumbe wa kibiashara bila ruhusa isipokuwa iwe maudhui yote yaliyomo uliyatengeneza wewe mwenyewe. Ukurasa wa vidokezo vya hakimiliki na Mwogozo wa Jumuiya unaweza kukusaidia kuamua kama video yako inakiuka hakimiliki za mtu mwingine. [28]

Lisha ya ushauri huu, bado kuna vijisehemu vingi vya maonyesho ya televisheni,video za nyimbo na filamu katika YouTube. YouTube huwa haitazami video kabla ya kuzichapisha kwenye wavuti, ila hupatia jukumu wamiliki wa hakimiliki kutoa notisi ya uvunjaji chini ya sheria za Millennium Digital Copyright Act. Mashirika yakiwemo Viacom, Mediaset na Ligi kuu ya Uingereza yameandikisha kesi dhidi ya YouTube, yakidai kuwa imefanya juhudi kidogo mno kuzuia upakiaji wa nyenzo zenye hakimiliki. [29] [30] [31] Viacom, wanadai dola bilioni 1 za Kimarekani kama fidia ya uharibifu, huku ikisema kuwa alikuwa imepata zaidi ya vijisehemu ambavyo vinatokana na nyenzo 150,000 zake katika YouTube na ambavyo vimetazamwa zaidi ya mara bilioni 1.5. YouTube alijibu kwa kusema ya kwamba huwa "inaenda mbali zaidi ya mipaka yake kisheria katika kusaidia kulinda nyenzo za wamiliki na kazi zao". Tangu Viacom kuandikisha kesi yake, YouTube imeanizisha mfumo uitwao VideoID, ambao huangalia video zilizopakiwa dhidi ya hifadhidata ya maudhui yenye hakimiliki kwa lengo la kupunguza ukiukaji. [32] [33]

Mnamo Agosti 2008, mahakama ya Marekani iliamua ya kwamba wamiliki wa hakimiliki hawawezi kuagiza kuondolewa kwa faili iliyo katika wavuti bila kwanza kubainisha kuwa kupakiwa kwakwe kunaonyesha matumizi ya haki ya nyenzo hii[[]]. Kesi hii ilihusisha Stephanie Lenz kutoka Gallitzin, Pennsylvania, ambaye alikuwa ameunda video ya kinyumbani ya mwanawe wa kiume wa miaka 13 huku akicheza wimbo wa Prince "Let's Go Crazy" na kupakia video hii ya sekunde 29 kwa YouTube. [34]

Faragha

Mnamo Julai 2008, Viacom ilishinda uamuzi wa mahakama uliohitaji YouTube kutoa na kuipa data kuhusu tabia ya kila mtazamaji ambaye anatazama video kenye tovuti. Hatua hii ilisababisha wasiwasi kwamba tabia ya mtazamaji binafsi ingeweza kutambuliwa kwa anwani ya IP na majina yao ya kuingilia tovuti. Uamuzi huo ulitiliwa lawama na Electronic Frontier Foundation, ambayo iliita uamuzi huu wa mahakama kama "sera inayorundisha nyuma haki za ufaragha". [35] Jaji Louis Stantonwa Mahakama ya Wilaya aliutupilia mbali wasiwasi wa faragha kama "uvumi", na kuiamuru YouTube kukabidhi nyaraka zilizokaribia terabyte 12 za data. Jaji Stanton alikataa ombi la Viacom kwa YouTube kukabidhi chanzo kanuni za mfumo wake wa utafiti, akisema kuwa hakuna ushahidi kuwa YouTube ilichukulia ukiukaji wa hakimiliki kwa namna tofauti. [36] [37]

Maudhui yasiyofaa

YouTube pia imekabiliwa na upinzani juu ya maudhui ya kukera yaliyomo katika baadhi ya video zake. Ingawa sheria ya utumiaji wa YouTube hukataza kupakia kwa video ambayo ina uwezekano wa kuwa na nyenzo zisizofaa, YouTube huwa haiangali kila video kabla ya kuwekwa kwenye wavuti. Sehemu zenye utata katika video zinahusisha ukanaji wa Mauaji ya Holocaust na mkasa wa Hillsborough, ambapo mashabiki 96 kutoka Liverpool waliangamizwa mwaka wa 1989, kwenye njama za kidhahania na dini. [38] [39]

YouTube hutegemea watumiaji wake kuonyesha ishara kuhusu maudhui ya video kama ni yale yasiyofaa, na wafanyakazi wa YouTube watatazama video iliyoashiriwa kubaini kama inakiuka mkataba wa masharti ya utumizi wa tovuti. [3] Mnamo Julai 2008 Kamati ya Utamaduni na Vyombo vya habari ya Bunge la Umoja la Uingereza ilisema ya kwamba ilikuwa "haijaridhishwa" na mfumo wa YouTube wa kutoa sera za video zake, na kujadili kuwa "kukabiliwa awali kwa maudhui yafaa kuwa kigezo cha sera ya tovuti kupakia [[maudhui yanayotoka kwa watumiaji|maudhui yanayotoka kwa watumiaji." YouTube alijibu kwa kusema kuwa: "Tuna sheria kali juu ya kile kinachoruhusiwa, na mfumo unaowezesha mtu yeyote ambaye anaona maudhui yasiyofaa kuripoti kwetu 24 / 7 kwa timu yetu na suala hili kushughulikiwa mara moja. Sisi huelimisha jamii yetu juu ya sheria na inahusisha kiungo cha moja kwa moja kutoka kwa kila ukurusa wa YouTube ili kurahisisha mchakato huu kama iwezekanavyo kwa watumiaji wetu. Kutokana na idadi kumbwa ya maudhui yaliyo pakiwa kwenye tovuti yetu, tunadhani kuwa hadi sasa hii ndiyo njia yenye ufanisi zaidi ili kuhakikisha kuwa video chache ambazo huvunja kanuni zinashuka haraka. [40]

Kuziba

Nchi kadhaa zimeziba upatikanaji wa YouTube tangu kuanzishwa kwake, ikiwemo Jamhuri ya Uchina, [41] [42] Morocco, [43] na Thailand. [44] YouTube sasa imezibwa nchini Uturuki baada ya utata juu ya video iliyoonekana kuwa yenye matusi kwa Mustafa Kemal Atatürk. [45] Licha ya kuzibwa huku, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alikubali kwa waandishi wa habari kwamba angeweza kupata YouTube, kwani tovuti bado inapatikana huko Uturuki kwa kutumia mbadala wa wazi. [46]

Tarehe 3 Desemba 2006, Iran iliziba kwa muda upataji wa YouTube, pamoja na tovuti zingine kadhaa, baada ya kuzitangaza kama zinazokiuka maadili ya kijamii na kanuni za vitendo. YouTube ilizibwa baada ya video iliyopakiwa kwenye wavuti kujaribu kumwonyesha Mwajemi/Mwirani anayeiigiza katika filamu za mapenzi akishiriki katika ngono. [47] Kuzibwa huku baadaye kuliondolewa na kisha kukarejeshwa Uajemi baada ya uchaguzi wa rais 2009. [48]

Mnamo 23 Februari 2008, Pakistan iliziba YouTube kutokana na "nyenzo za kukera" kwa imani ya Uislamu , pamoja na kuonyeshwa kwa katuni ya Kideni ya nabii Muhammad. [49] Hii ilisababisha karibu kuzimwa kimataifa kwa tovuti ya YouTube karibu masaa mawili, kwa vile kuzibwa huko kwa Pakistan kulichukuliwa na nchi nyingine. Pakistan iliondoa kizibo chake tarehe 26 Februari 2008. [50] Wapakistani walizunguka kizibo hicho cha siku tatu kwa kutumia programu mtandao wa kibinafsi. [[]]. [51]

Shule katika baadhi ya nchi zimeziba upatikanaji wa YouTube kutokana na wanafunzi wa kupakia video zenye tabia ya uchokozi, vita vya shuleni,tabia ya ubaguzi wa rangi, na nyenzo zingine zisizofaa. [52]

Teknolojia

Ulinganifu wa kawaida, juu, na HD wa ubora wa video za YouTube zikichezwa katika YouTube na uimarisho wa asili wa video hizi.

Muundo wa video

Teknologia ya urejeshi wa kucheza Video za YouTube kwa watumiaji wa mtandao inatokana na Adobe Flash Player. Hii inaruhusu tovuti kuonyesha video bora ikilinganishwa na teknolojia zilizoimarika za kucheza video (kama Windows Media Player, QuickTime, na RealPlayer) ambazo kwa ujumla huhitaji mtumiaji kupakua na kuweka programu-jalizi kwa kivinjari ili kutazama maudhui ya video. [53] Kutazama video ya Flash pia kunahitaji plogramu-jalizi, lakini utafiti wa soko kutoka kwa Adobe Systems umegundua ya kwamba plogramu-jalizi yake imewekwa kwa Kiwango cha asilimia 95 kwenye kompyuta za kibinafsi. [54]

Video zilizopakiwa kwa YouTube kutoka kwa wamiliki maalum wa akaunti zafaa kuwa na urefu wa dakika kumi na faili ya kiasi cha GB [55] 2.[56] Wakati YouTube ilipozinduliwa mwaka wa 2005 kulikuwa na uwezekano wa kupakia video ndefu, lakini upeo wa dakika kumi ulianzishwa Machi 2006 baada ya YouTube kugundua kwamba nyingi ya video zilizozidi urefu huu zilikuwa na maudhui yasiyoruhusiwa ya maonyesho ya televisheni na filamu. [57] [58] Akaunti za ushirika zinaruhusiwa kupakiwa kwa video zenye urefu wa zaidi ya dakika kumi, lakini kwa kukubaliwa na YouTube. [59]

YouTube inapokea video zilizopakiwa katika miundo mingi, ikiwa pamoja na.[[WMV,.|WMV,.]][[AVI,.|AVI,.]][[MKV,.|MKV,.]]MOV, [[MPEG,.|MPEG,.]]MP4, [[DivX,.|DivX,.]]FLV, na.OGG. Pia inaruhusu 3gp, na kuruhusu video kupakiwa moja kwa moja kutoka kwa simu ya mkononi. [60]

Ubora wa video

YouTube awali ilitoa video katika muundo mmoja tu, lakini sasa ina miundo mikuu mitatu, vilevile muundo wa "simu za mkononi", wa kutazamwa kwenye simu za mkononi. Muundo asili, sasa una kibali cha "ubora wa wastani", huonyesha video kwa uimarisho wa pixel 320x240 kwa kutumia Spark Sorenson Codec, pamoja na mono MP3 audio. [61] Hii ilikuwa, kwa wakati huo, kiwango cha wastani cha kutazama video kwenye wavuti.

Video za "ubora wa juu", zilizoanzishwa Machi 2008, huonyeshwa hadi kwa pixels 864x480 na sauti ya stereo AAC. [62] Muundo huu huwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha kiwango cha wastani cha ubora. Mwezi Novemba 2008 720p HD ya kuwezesha zaidi iliongezwa. [63] Wakati huo huo, kifaa cha kucheza video cha YouTube kilibadilishwa kutoka kwa 4:3 kipengele cha uwiano hadi kwa kiwambo kipana. 16:9Video za 720p huwa zinaonyeshwa kwa uimarisho wa pixel 1280x720, uimarisho huu ukiwa umetengenezwa na H.264 video Codec. Pia hili linahusisha stereo audio ikiwa imetengenezwa na AAC.

Utazamaji wa video kwa njia ya 3D

Katika video iliyochapishwa mnamo 21 Julai 2009, [64] mhandisi wa plogramu wa YouTube Peter Bradshaw alitangaza kuwa watumiaji wa YouTube sasa wangeweza kupakia video za aina ya 3D. Video hizi zinaweza kutazamwa kwa njia ya kawaida, na miwani huvaliwa na watazamaji ili kupata athari ya 3D. [65] [66] [67]

Upatikanaji wa matini

Mojawapo ya sifa za YouTube ni uwezo wa watumiaji kutazama video zake katika tovuti nje ya wavuti wake. Kila video ya YouTube huandamana pamoja na kipande cha HTML, ambacho chaweza kutumika kuiweka kwenye ukurasa nje ya tovuti ya YouTube. Utendakazi huu mara nyingi hutumika kuweka video za YouTube katika kurasa za mitandao ya kijamii na blogu. [68]

YouTube kawaida huwa haitoi kiungo cha kupakua video zake, na hutarajia kuwa huwa zinatazamwa kupitia kwa kusano la tovuti yake. [69] Idadi ndogo ya video, kama vile hotuba ya rais Barack Obama, inaweza kupakuliwa kama faili za MP4. [70] Wavuti mbalimbali za mrengo wa tatu, na vifaa vya matumizi na plogramu-jalizi za kivinjari huruhusu watumiaji kupakua video za YouTube. [71] Mnamo Februari 2009, YouTube ilitangaza huduma ya majaribio, ya kuruhusu baadhi ya washirika kutoa upakuaji wa video bure au kwa malipo ya ada kwa njia ya Google Checkout. [72]

Majukwaa

Baadhi ya simujanja zina uwezo wa kupata video za YouTube, kutegemea mtoaji na mpango wa data. Simu ya YouTube ilizinduliwa mwezi Juni 2007, na hutumia RTSP ili kutazama video. [73] Si video zote za YouTube zinazopatikana kwenye muundo wa tovuti ya simu. [74]

Tangu Juni 2007,video za YouTube huwa zinapatikana kwa ajili ya kutazamwa katika bidhaa mbalimbali za Apple. Hii ilihitaji matini ya YouTube kubadilishwa hadi katika kiwango wastani kinachopendelewa cha Apple, H.264, mchakato uliochukua miezi kadhaa. Video za YouTube huweza kutazamwa kwa kutumia vifaa vikiwemo Apple TV na iPhone. [75] Huduma ya TiVoiliyoboreshwa mnamo Julai 2008 iliruhusu mfumo huu kutafuta na kucheza video za YouTube. [76] Mnamo Januari 2009, YouTube ilizindua "YouTube ya TV", na ni toleo la tovuti ya inayolenga mfumo wa set-top boxes na vyombo vingine vya habari vinavyohusu vifaa vya TV vyenye vivinjari, mwanzo, zikiruhusu video zake kutazamwa katika PlayStation 3 na Wii video game console s. [77] [78] Mwezi Juni 2009, YouTube XL ilitolewa, ambayo ina kusano iliyorahisishwa, iliyoundwa kwa ajili ya kutazama kwenye televisheni yenye kiwamgo cha wastani. [79]

Ujanibishaji

19 Juni 2007, Msimamizi mkuu wa Google Eric E. Schmidt alikuwa mjini Paris kuzindua mfumo mpya wa ujanibishaji. [80] Kusano zima la tovuti hii sasa linapatikana kwa mifumo iliyo fanyiwa ujanibishaji katika nchi 22:

Nchi URL Lugha: Tarehe ya Uzinduzi
Bendera ya Australia Australia au.youtube.com Kiingereza (Australia) 02007-10-22 22 Oktoba 2007[81]
Bendera ya Brazil Brazil br.youtube.com Kireno (Brazil) 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Kanada Kanada ca.youtube.com Kiingereza (Kanada) na Kifaransa (Kanada) 02007-11-06 6 Novemba 2007[82]
Bendera ya Ucheki Czech Republic cz.youtube.com Kicheki 02008-10-09 9 Oktoba 2008[83]
Bendera ya Ufaransa Ufaransa fr.youtube.com Kifaransa 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Ujerumani Ujerumani de.youtube.com Kijerumani 02007-11-08 8 Novemba 2007[84]
Bendera ya Hong Kong Hong Kong hk.youtube.com Kichina (cha Kiasili) 02007-10-17 17 Oktoba 2007[85]
Bendera ya Israel Israel il.youtube.com Kiingereza 02008-09-16 16 Septemba 2008
Bendera ya Uhindi India in.youtube.com Kiingereza (Uhindi) na Kihindi 02008-05-07 7 Mei 2008[86]
Bendera ya Eire Ireland ie.youtube.com Kiingereza (Ayalandi) 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Italia Italy it.youtube.com Kiitaliano 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Japani Japan jp.youtube.com Kijapani 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya South Korea Korea Kusini kr.youtube.com Kikorea 02008-01-23 23 Januari 2008
Bendera ya Mexiko Meksiko mx.youtube.com Kihispania (Mexico) 02007-10-10 10 Oktoba 2007
Bendera ya Uholanzi Uholanzi nl.youtube.com Kidachi 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya New Zealand New Zealand nz.youtube.com Kiingereza (Nyuzilandi) 02007-10-22 22 Oktoba 2007[81]
Bendera ya Poland Poland pl.youtube.com kipolandi 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Urusi Urusi ru.youtube.com Kirusi 02007-11-13 13 Novemba 2007
Bendera ya Hispania Hispania es.youtube.com Kihispania 02007-06-19 19 Juni 2007[80]
Bendera ya Uswidi Uswidi se.youtube.com Kiswidi 02008-10-22 22 Oktoba 2008
Bendera ya Jamhuri ya China Taiwani tw.youtube.com Kichina (cha Kiasili) 02007-10-18 18 Oktoba 2007[85]
Bendera ya Ufalme wa Muungano Ufalme wa Muungano uk.youtube.com Kiingereza (Uingereza) 02007-06-19 19 Juni 2007[80]

Hivi karibuni imeanzishwa Youtube kwa lugha ya Kiswahili.

Kusano la YouTube hupendekeza mfumo ambao unapaswa kuchaguliwa kwa kuzingatia anwani ya IP ya mtumiaji. Katika baadhi ya matukio, ujumbe "Video hii haipatikani katika nchi yako" waweza kuonekana kutokana na vikwazo vya hakimiliki au maudhui yasiyofaa. [87]

Mipango ya YouTube ya kuunda toleo huko Uturuki imepatwa na matatizo, tangu mamlaka ya Kituruki ilipoihitaji YouTube kuanzisha ofisi huko Uturuki, ambayo ingekuwa chini ya sheria za Kituruki. YouTube anasema kwamba haina nia ya kufanya hivyo, na kwamba video zake haziko chini ya sheria za Kituruki. Mamlaka ya Kituruki yameonyesha wasiwasi kuwa YouTube imetumika kupakia video zenye matusi kwa Mustafa Kemal Atatürk na baadhi ya nyenzo zake ni zakukera kwa Waislamu [88] [89]

Mwezi Machi 2009, mabishano kati ya YouTube na wakala wa ukusanyaji wa asilimia ya mapato ya muziki[[]] Uingereza [[]] PRSP walisababisha video za premia kuzibwa kwa watumiaji wa YouTube nchini Uingereza. Kuondolewa kwa video zilizopakiwa na makampuni makubwa ya kurekodi kulitokea baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mpango wa leseni. Mgogoro huu ulitatuliwa Septemba 2009. [90] Mwezi Aprili 2009, mzozo kama huo ulisababisha kuondolewa kwa video za nyimbo zenye kulipiwa kwa watumiaji kutoka Ujerumani. [91]

Angalia pia

Marejeo

  1. Hopkins, Jim. "Surprise! There's a third YouTube co-founder". USA Today. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  2. Weber, Tim. "BBC strikes Google-YouTube deal". BBC. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  3. 3.0 3.1 "YouTube Community Guidelines". YouTube. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  4. Graham, Jefferson (2005-11-21). "Video websites pop up, invite postings". USA Today. Iliwekwa mnamo 2006-07-28.
  5. "YouTube: Sharing Digital Camera Videos". University of Illinois at Urbana-Champaign. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-11. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  6. Cloud, John. "The Gurus of YouTube". Time Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-19. Iliwekwa mnamo 2008-11-29. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  7. Miguel Helft and Matt Richtel. "Venture Firm Shares a YouTube Jackpot". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  8. Sara Kehaulani Goo. "Ready for Its Close-Up". Washington Post. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  9. "Whois Record for www.youtube.com". DomainTools. Iliwekwa mnamo 2009-04-01.
  10. Alleyne, Richard. "YouTube: Overnight success has sparked a backlash". Daily Telegraph. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  11. "Me at the zoo". YouTube. 2005-04-23. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  12. "YouTube serves up 100 million videos a day online". USA Today. 2006-07-16. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  13. "YouTube Surpasses 100 Million U.S. Viewers for the First Time". comScore. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-05. Iliwekwa mnamo 2009-03-05.
  14. Junee, Ryan (2009-05-20). "Zoinks! 20 Hours of Video Uploaded Every Minute!". YouTube. Iliwekwa mnamo 2009-05-26.
  15. "Eric Schmidt, Princeton Colloquium on Public & Int'l Affairs". YouTube. Iliwekwa mnamo 2009-06-01.
  16. "Web could collapse as video demand soars". Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-08. Iliwekwa mnamo 2008-04-21.
  17. Yen, Yi-Wyn (2008-03-25). "YouTube Looks For the Money Clip". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-17. Iliwekwa mnamo 2008-03-26.
  18. "Alexa Traffic Rank for YouTube (three month average)". Alexa Internet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-27. Iliwekwa mnamo 2009-08-26.
  19. Zappone, Christian. "Help! YouTube is killing my business!". CNN. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  20. Blakely, Rhys. "Utube sues YouTube". The Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-09. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  21. Brad Stone and Brooks Barnes. "MGM to Post Full Films on YouTube". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2008-11-29.
  22. Staci D. Kramer (2009-04-30). "It's Official: Disney Joins News Corp., NBCU In Hulu; Deal Includes Some Cable Nets". paidContent.org. Iliwekwa mnamo 2009-04-30. {{cite news}}: Unknown parameter |dateformat= ignored (help)
  23. Bray, Marianne. "Irate HK man unlikely Web hero". CNN. Iliwekwa mnamo 2008-05-28.
  24. "guitar". YouTube. 2005-12-20. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  25. Heffernand, Virginia (2006-08-27). "Web Guitar Wizard Revealed at Last". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2007-07-02.
  26. "Complete List of 2008 Peabody Award Winners". Peabody Awards, University of Georgia. 2009-04-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-08. Iliwekwa mnamo 2009-04-01.
  27. Ho, Rodney (20009-04-02). "Peabody honors CNN, TMC". Atlanta Journal-Constitution. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-28. Iliwekwa mnamo 2009-04-14. {{cite news}}: Check date values in: |date= (help)
  28. Marsden, Rhodri (2009-08-12). "Why did my YouTube account get closed down?". The Independent. Iliwekwa mnamo 2009-08-12.
  29. "Viacom will sue YouTube for $1bn". BBC News. Iliwekwa mnamo 2008-05-26.
  30. "Mediaset Files EUR500 Million Suit Vs Google's YouTube". CNNMoney.com. 30 Julai 2008. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2009.
  31. "Premier League to take action against YouTube". Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-17. Iliwekwa mnamo 2008-05-24.
  32. "YouTube law fight 'threatens net'". BBC News. Iliwekwa mnamo 2008-05-28.
  33. Allen, Katie. "Google seeks to turn a profit from YouTube copyright clashes". The Guardian. Iliwekwa mnamo 2009-11-02.
  34. "Woman can sue over YouTube clip de-posting". San Francisco Chronicle. 2008-08-20. Iliwekwa mnamo 2008-08-25. {{cite news}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  35. "Google must divulge YouTube log". BBC News. Iliwekwa mnamo 2008-07-03.
  36. "YouTube ordered to reveal its viewers". CNN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-07. Iliwekwa mnamo 2008-07-04.
  37. Helft, Miguel. "Google Told to Turn Over User Data of YouTube". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2008-07-04.
  38. "YouTube criticized in Germany over anti-Semitic Nazi videos". Reuters. Iliwekwa mnamo 2008-05-28.
  39. "Fury as YouTube carries sick Hillsboro video insult". icLiverpool. Iliwekwa mnamo 2008-05-24.
  40. "YouTube attacked by MPs over sex and violence footage". Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-07. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
  41. Schwankert, Steven. "YouTube finally back online in China". PC Advisor. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-06. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  42. Sommerville, Quentin. "China 'blocks YouTube video site'". BBC News. Iliwekwa mnamo 2009-03-24.
  43. Richards, Jonathan. "YouTube shut down in Morocco". The Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-09. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  44. "Thailand blocks access to YouTube". BBC. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  45. Rosen, Jeffrey (2008-11-30). "Google's Gatekeepers". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2008-12-01. {{cite news}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  46. Doğan News Agency. "Ban on YouTube proves virtual". Hürriyet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  47. "Censorship fears rise as Iran blocks access to top websites". 4 Novemba 2006. Iliwekwa mnamo 2006-12-17. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  48. "Mobile phones, Facebook, YouTube cut in Iran". American Free Press. Google. 13 Julai 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-18. Iliwekwa mnamo 2009-07-08. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  49. "Pakistan blocks YouTube website". BBC. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  50. "Pakistan lifts the ban on YouTube". BBC. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  51. "Pakistan web users get round YouTube ban". Silicon Republic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-29. Iliwekwa mnamo 2008-11-30.
  52. Colley, Andrew (2007-03-06). "States still hold out on YouTube". Australian IT. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-23. Iliwekwa mnamo 2009-12-01. {{cite news}}: Text "accessdate2007-10-11" ignored (help)
  53. Atwood, Jeff. "Did YouTube Cut the Gordian Knot of Video Codecs?". Coding Horror. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-02. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
  54. "Adobe Flash Player Version Penetration". Adobe Systems. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
  55. Baker, Loren (2006-03-31). "YouTube 10 Minute Limit Deters Copyrighted Video Uploads". Search Engine Journal. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  56. "YouTube doubles video file size to 2G". AFP. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-09. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
  57. Fisher, Ken. "YouTube caps video lengths to reduce infringement". Ars Technica. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
  58. "Account Types: Longer videos". YouTube. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
  59. "How do I upload a video longer than ten minutes?". YouTube. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-12. Iliwekwa mnamo 200-08-21. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  60. "Video Formats: File formats". YouTube. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
  61. "Market Deamnd for Sorenson Media's Sorenson Spark Video Decoder Expands Sharply". Sorenson Media. 2009-06-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-27. Iliwekwa mnamo 2009-07-31.
  62. "YouTube Blog - YouTube Videos in High Quality". YouTube. 2008-03-24. Iliwekwa mnamo 2009-04-04.
  63. "Bigger Isn't Always Better... But in This Case, We Believe It Is". YouTube Blog. YouTube. 2008-11-25. Iliwekwa mnamo 2009-04-04.
  64. "YouTube in 3D". YouTube. 2009-07-21. {{cite web}}: |access-date= requires |url= (help); Missing or empty |url= (help); Unknown parameter |http://www.youtube.com/watch?v= ignored (help)
  65. Marquit, Miranda (2009-07-23). "YouTube in 3D?". Physorg. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  66. Dsouza, Keith (2009-07-20). "YouTube 3D Videos". Techie Buzz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-02. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  67. Sobti, Kshitij (2009-07-21). "YouTube adds a dimension, 3D goggles not included". thinkdigit. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  68. YouTube. "Sharing YouTube Videos". Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  69. "Terms of Use, 6.1". YouTube. Iliwekwa mnamo 2009-02-20.
  70. CNET (2009-01-16). "(Some) YouTube videos get download option". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-18. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  71. Milian, Mark (2009-02-19). "YouTube looks out for content owners, disables video ripping". Los Angeles Times. Iliwekwa mnamo 2009-02-21.
  72. "YouTube Hopes To Boost Revenue With Video Downloads". Washington Post. 2009-02-12. Iliwekwa mnamo 2009-02-19.
  73. "YouTube Mobile".
  74. Google Operating System (2007-06-15). "Mobile YouTube". Iliwekwa mnamo 2009-01-17. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  75. "YouTube Live on Apple TV Today; Coming to iPhone on June 29". Apple. 2007-06-20. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  76. "TiVo Getting YouTube Streaming TODAY". Gizmodo. 2007-07-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-12. Iliwekwa mnamo 2009-02-17.
  77. "YouTube video comes to Wii and PlayStation 3 game consoles". Los Angeles Times. 2009-01-15. Iliwekwa mnamo 2009-01-17.
  78. "Coming Up Next... YouTube on Your TV". YouTube Blog. 2009-01-15. Iliwekwa mnamo 2009-05-10.
  79. "Experience YouTube XL on the Big Screen". YouTube Blog. YouTube. 2009-06-02. Iliwekwa mnamo 2009-06-20.
  80. 80.00 80.01 80.02 80.03 80.04 80.05 80.06 80.07 80.08 80.09 Sayer, Peter (2007-06-19). "Google launches YouTube France News". PC Advisor. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  81. 81.0 81.1 Nicole, Kristen (2007-10-22). "YouTube Launches in Australia & New Zealand". Mashable. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  82. Nicole, Kristen (2007-11-06). "YouTube Canada Now Live". Mashable. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  83. Bokuvka, Petr (2008-10-12). "Czech version of YouTube launched. And it's crap. It sucks". The Czech Daily Word. Wordpress.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  84. Ostrow, Adam (2007-11-08). "YouTube Germany Launches". Mashable. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  85. 85.0 85.1 "Chita • 檢視主題 - YouTube 台灣版推出". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2009-12-01.
  86. Joshi, Sandeep (2008-05-08). "YouTube now has an Indian incarnation". The Hindu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-28. Iliwekwa mnamo 2009-08-03.
  87. "Learn More: Video not available in my country". YouTube Help. Iliwekwa mnamo 2009-08-04.
  88. "Long-standing YouTube ban lifted only for several hours". Today's Zaman. 2008-06-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-04. Iliwekwa mnamo 2008-07-10.
  89. Danforth, Nick (2009-07-31). "Turks censor YouTube censorship". San Francisco Chronicle. Iliwekwa mnamo 2009-08-04.
  90. Barnett, Emma (2009-09-03). "Music videos back on YouTube in multi-million pound PRS deal". Daily Telegraph. Iliwekwa mnamo 2009-09-03.
  91. "Now YouTube stops the music in Germany". The Guardian. 2009-04-01. Iliwekwa mnamo 2009-04-02.

Kusoma zaidi

  • Lacy, Sarah: The Stories of Facebook, YouTube and MySpace: The People, Hype and Deals behind Giants of web the 2,0 (2008) ISBN 978-1-85458-453-3

Viungo vya nje

Jua habari zaidi kuhusu YouTube kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi
Vitabu kutoka Wikitabu
Dondoo kutoka Wikidondoa
Matini za vyanzo kutoka Wikichanzo
Picha na media kutoka Commons
Habari kutoka Wikihabari
Vyanzo vya elimu kutoka Wikichuo