Visiwa vya Sunda
Mandhari
Visiwa vya Sunda ni sehemu ya funguvisiwa la Malay katika Bahari Hindi. Kwa kawaida vinatofautishwa kati ya Visiwa Vikubwa vya Sunda na Visiwa Vidogo vya Sunda. Sumatra, Java, Borneo na Sulawesi hufanya Visiwa Vikubwa vya Sunda. Visiwa vidogo vya Sunda vinajumlisha visiwa vingi vidogo.
Leo, Visiwa vya Sunda vimegawanywa kati ya nchi za Indonesia, Malaysia, Brunei na Timor ya Mashariki .
Ndani ya visiwa hivyo kuna mpaka wa kiekolojia inayoitwa "mstari wa Wallace". Mstari huu unatenganisha mimea na wanyama wa Asia na wale wa Australia.
Laini ya Wallace pia inaendesha kupitia Visiwa vya Sunda. Ni mgawanyiko wa kibiolojia kati ya fauna na mimea ya Australia, na ile ya Asia ya Kusini.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Sunda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |