Nenda kwa yaliyomo

Uswisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Schweizerische Eidgenossenschaft
Confédération suisse
Confederazione Svizzera
Confederaziun svizra
Confoederatio Helvetica
Shirikisho la Uswisi
Bendera ya Uswisi Nembo ya Uswisi
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: Unus pro omnibus, omnes pro uno
(Kiswahili: "Mmoja kwa ajili ya wote - wote kwa ajili ya mmoja")
Wimbo wa taifa: Zaburi ya Uswisi
Lokeshen ya Uswisi
Mji mkuu Bern (mji mkuu wa shirikisho)
46°57′ N 7°27′ E
Mji mkubwa nchini Zürich
Lugha rasmi Kijerumani, Kifaransa, Kiitalia, Kirumanj[1]
Serikali
Halmashauri ya Shirikisho
kwa jumla ni Mkuu wa Dola
Mwenyekiti wa mawaziri
ana cheo cha "Rais"
akibadilika kila mwaka
Demokrasia, Shirikisho la Jamhuri
Viola Amherd
(Rais wa Shirikisho mwaka 2024)
Karin Keller-Sutter (VP)
Guy Parmelin
Ignazio Cassis
Albert Rösti
Elisabeth Baume-Schneider
Beat Jans
Uhuru
Imetangazwa
Imekubaliwa
Shirikisho la Jamhuri

1 Agosti 1291
1648
1848
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
41,285 km² (ya 132)
4.2
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,570,146 (ya 99)
8,139,600
207/km² (ya 48)
Fedha Swiss franc (CHF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .ch
Kodi ya simu +41

-



Uswisi ni nchi ya Ulaya isiyo na pwani katika bahari yoyote.

Imepakana na Ujerumani, Ufaransa, Italia, Austria na Liechtenstein.

Jina rasmi ni Confoederatio Helvetica (kwa Kilatini: Shirikisho la Kiswisi).

Majimbo yake 26, ambayo huitwa "kantoni", yanajitawala.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Shirikisho la Uswisi lilianza mwaka 1300 hivi kutokana na ushindi vitani dhidi ya Austria na Burgundy.

Uhuru wa shirikisho kutoka Dola Takatifu la Kiroma ulitambuliwa rasmi katika Amani ya Westphalia mwaka 1648.

Uswisi imepata umaarufu hasa kutokana na sababu zifuatazo:

Ramani

Mji mkuu wa shirikisho ni Bern.

Mji mkubwa ni Zürich wenye benki nyingi.

Mji wa Geneva ni kati ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa; ni pia makao makuu ya kimataifa ya Umoja wa shirika za Msalaba Mwekundu na mashirikia mengine ya kimataifa.

Hata hivyo Uswisi imekuwa kati ya nchi za mwisho kujiunga na UM (2002).

Kuna lugha rasmi 4: Kijerumani (62.8%), Kifaransa (22.9%), Kiitalia (8.2%) na Kirumanj (0.5%). Lakini wengi wanajua na kutumia lugha zaidi ya moja.

Kati ya lugha za kigeni zinazotumika nyumbani, zinaongoza Kiingereza (5%), Kireno (3.8%), Kialbania (3%), Kihispania (2.6%), Kiserbokroatia (2.5%) n.k.

Upande wa dini, kati ya wakazi, 68% ni Wakristo, hasa Wakatoliki (37.2%) na Wakalvini (25%), lakini pia Waorthodoksi (2.3%) na wengineo. 5.1% ni Waislamu (hasa wahamiaji). 24% hawana dini maalumu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Switzerland Constitution, article 70, "Languages": (1) The official languages of the Federation are German, French, and Italian. Romansh is an official language for communicating with persons of Romansh language. (2) The Cantons designate their official languages. In order to preserve harmony between linguistic communities, they respect the traditional territorial distribution of languages, and take into account the indigenous linguistic minorities.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Uswisi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uswisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.