Ufunguo
Ufunguo (kutoka kitenzi "kufunga", kinyume chake "kufungua") ni kifaa kinachotumika kufungulia au kufungia mlango, kufuli n.k.
Kwa sababu hiyo, mara nyingi huchukuliwa kama ishara ya kumiliki nyumba, sanduku n.k. Mwambatanisho wa kufuli na ufunguo huchangia katika ulinzi kwa maana ni mwenye ufunguo peke yake anayeweza kufungua kitasa au kufuli.
Historia ya ufunguo
[hariri | hariri chanzo]Historia ya ufunguo inafanana na ile ya kufuli maana zote zilitengenezwa kwa pamoja. Kufuli na ufunguo wa kwanza zilipatikana kule Ninawi, Assyria.[1] Baadaye, mwambatanisho huo ulipatikana nchini Misri.[2]
Baada ya mfumo huu wa ulinzi kuitikiwa na wote, uvumbuzi uliendelezwa na teknolojia pia kutumika katika kuboresha kufuli na funguo.
Leo, funguo za kisasa zahitilafiana sana na zile za zamani. Hata hivyo, minajili ni ilele: ulinzi.
Funguo za kisasa
[hariri | hariri chanzo]Funguo za leo zina ulinzi mwingi kuliko ule wa zamani. Wezi waliweza kufungua na kuingia kwenye nyumba za kufuli za kitambo maana zilitengenezwa kwa teknolojia dhaifu.
Hivi leo, teknolojia ni nzuri na ni vigumu (hata kama bado itafanyika) kufungua kufuli kwa ufunguo usiodhaminiwa kufanya hivyo. Pia kuna teknolojia ambayo inazuia mtu kutengeneza nakala ya ufunguo bila ruhusa ya mwenye ufunguo.
Pia kumekuwa na kufuli zisizohitaji ufunguo wa kawaida bali tu kubofya nambari. Milango hii ni kama ile ya karakana za gari, ya milango ya nyumba na kampuni.
Kuna milango pia ambayo hufunguliwa kwa njia ya kieletroniki baada ya kutambua anayejaribu kufungua.
Funguo na taaluma ya lokismithi
[hariri | hariri chanzo]Upotevu wa funguo au kuvunjika kwa funguo hufanya mtu ateseke sana akijaribu kuufungua au hata kuuvunja mlango. Kwa kuepuka hii shida, watu wengi huona heri waende kwa walio na taaluma ya lokismithiambayo ni taaluma ya kutengeneza funguo, kufuli na usalama wote wa kinyumbani. Lokismithi hawa huweza kuifungua ile milango kwa kutengeneza funguo badala au kuikata kufuli.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ de Vries, N. Cross and D. P. Grant, M. J. (1992). Design Methodology and Relationships with Science: Introduction. Eindhoven: Kluwer Academic Publishers. uk. 32. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Aprili 2016.
{{cite book}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Ceccarelli, Marco (2004). International Symposium on History of Machines and Mechanisms. New York: Kluwer Academic Publishers. uk. 43. ISBN 1402022034. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Aprili 2016.
{{cite book}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |