Tuta la mchanga
Tuta la mchanga ni kilima cha mchanga kilichojengwa na upepo kwa kupuliza na kusukuma punje za mchanga. Kama halishikwi na mimea inaweza kuhamahama.
Matuta ya mchanga hutokea penye mchanga usiofunikwa na udongo au mimea ya kutosha.
Mifano ni:
- Kando la bahari: mahali pengi ufukoni ni kawaida kuwa na mstari mmoja au miwili ya matuta ya mchanga kando la maji.
- Jangwani: penye jangwa la mchanga maeneo makubwa yanaweza kutokea kama matuta ya mchanga.
Matuta ya mchanga ni hatari kwa ajili ya binadamu kwa sababu yanaweza kufunika mashamba, nyumba hata kijiji kizima. Kama upepo ni mkali yanaweza kuhama mita makumi kila nafasi ya dhoruba.
Kuna majaribio mengi ya kusimamisha matuta yasihame. Njia mojawapo ni kupanda manyasi katika maeneo penye mvua wa kutosha. Hii ni kazi inayohitaji uangilifu. Lazima kurudia kupanda pale ambako majani yamekufa. Lazima kuzuia wanyama na watu wasikanyage kati ya manyasi haya.
Mradi wa kuhifadhi mazingira ya Umoja wa Mataifa unasaidia miradi ya aina hii kote duniani.