Taka
Taka au takataka (kwa Kiingereza: waste, trash, garbage, rubbish, junk) ni mabaki ya vitu, pia yale yanayobaki baada ya kuzalisha vitu, pamoja na yale yaliyotumiwa tayari na ambayo hayana matumizi tena.
Takataka ni kila dutu inayotupwa baada ya matumizi yake, au yenye kasoro na kwa hiyo haiwezi kutumika tena. Takataka hutupwa.
Neno
[hariri | hariri chanzo]Taka au takataka inamaanisha kiasili uchafu, kinachotupwa, kinachofagiwa, au pia vitu vidogo vya shamba visivyo na thamani kubwa[1].
Aina za takataka
[hariri | hariri chanzo]Takataka inaweza kutokea kwa hali mango au kiowevu. Gesi chafu kwa kawaida haihesabiki kati ya takataka, isipokuwa gesi iliyobaki katika vyombo pamoja na vyombo vile.
Hasara za taka
[hariri | hariri chanzo]Taka zina athari nyingi katika jamii. Athari hizo niː
- 1. Taka husababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya manjano, minyoo, kansa n.k. hasa zikitokea karibu na makazi ya watu.
- 2. Husababisha uharibifu wa mazingira: hufanya mazingira kuwa machafu.
- 3. Taka husababisha uharibifu wa maji, misitu n.k.
- 4. Taka zikichomwa hutoa moshi ambao husababisha uharibifu wa tabaka la ozoni ambalo ni muhimu kwa kupunguza mwanga wa jua kufikia kwenye ardhi ya dunia.
Hivyo tunashauriwa kutupa taka kwenye mashimo na kisha kuzichoma moto ili zisije zikaleta madhara kwenye jamii.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ linganisha Krapf (1882), "taka", pia Madan (1903)
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Taka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |