Nenda kwa yaliyomo

Suvorexant

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Suvorexant, inayouzwa kwa jina la kibiashara Belsomra, ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya kulala, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kusinzia na kusalia usingizini.[1] Dawa hii inaweza kuwa na ufanisi kwa angalau mwaka mmoja[1] na inachukuliwa kwa njia ya mdomo, nusu saa kabla ya kulala.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi usingizi, maumivu ya kichwa, ndoto zisizo za kawaida, kikohozi na kinywa kikavu.[1] Madhara yake mengine ni pamoja na matumizi mabaya ya madawa, kupooza wakati wa kulala au kuamka, kujiua, wasiwasi na uwezo mdogo wa kuendesha gari.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito na kunyonyesha hauko wazi.[2] Dawa hii ni kipinzani cha kipokezi cha orexin (orexin receptor antagonist).[1]

Suvorexant iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2014, [1] na Kanada mwaka wa 2018. [3] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 380 za Marekani kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[4] Nchini Marekani, ni dutu inayodhibitiwa na Ratiba ya IV.[5]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Suvorexant Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Suvorexant (Belsomra) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Regulatory Decision Summary - Belsomra - Health Canada". hpr-rps.hres.ca. Government of Canada. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 6 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Suvorexant Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Rules - 2014 - Final Rule: Placement of Suvorexant into Schedule IV". www.deadiversion.usdoj.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-17. Iliwekwa mnamo 2016-04-03.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suvorexant kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.