Samuel Morse
Samuel Finley Breese Morse (Aprili 27, 1791 - Aprili 2, 1872) alikuwa mvumbuzi wa Marekani. Alibuni telegrafu ya kwanza yenye waya mmoja tu. Jina lake hukumbukwa hasa kwa ajili ya kubuni alfabeti ya Morse.
Tangu miaka ya 1700, kulikuwa na aina tofauti za telegrafu zilizotumia nyaya nyingi. Morse alitumia miaka kadhaa kubuni mashine iliyoweza kupeleka ujumbe kwa kutumia waya mmoja tu, alichofaulu mnamo 1836. [1] Morse na msaidizi wake walibuni msimbo au alfabeti iliyoweza kuonyesha herufi zote kwa kutumia nukta na mistari pekee, ambazo ziliweza kutekelezwa kwa kubofya telegrafu.
Uvumbuzi wa Morse uliwezesha mawasiliano ya haraka na watu walio mbali. Hapo nyaya nyingi za telegrafu zilijengwa. Kati ya nyaya za kwanza za telegrafu ulikuwa ule uliojengwa kati ya Washington, DC na Baltimore nchini Marekani mnamo 1844. Kufikia miaka ya 1860, kulikuwa na nyaya za telegrafu kote baina ya miji ya Marekani, na mnamo 1866, waya wa kwanza wa telegrafu ulivuka Bahari ya Atlantiki. [2]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Samuel FB Morse alizaliwa huko Charlestown, Massachusetts.
Morse alikuwa mchoraji kabla ya kuwa mvumbuzi. Alikuwa profesa wa sanaa katika Chuo Kikuu cha New York. Alitaka kuchora picha kadhaa kwa ajili ya bunge la Marekani lakini hakukubaliwa kwa kazi hiyo. Alisikitishwa sana, hivi kwamba aliacha uchoraji akahamia uvumbuzi. [3]
Morse alikuwa Mkristo mwaminifu. Ujumbe wa kwanza aliotuma kwenye telegrafu yake ya 1844 ulikuwa "Je! Mungu ametenda nini?", ambayo ni nukuu hutoka Kitabu cha Hesabu katika Biblia.
Alifariki katika jiji la New York mnamo Aprili 2, 1872.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Inventor of the Week: Archive". web.mit.edu. Julai 2002. Iliwekwa mnamo Novemba 26, 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Samuel F. B. Morse Home Page". memory.loc.gov. Iliwekwa mnamo Novemba 26, 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McCullough, David (Septemba 2011). "Samuel Morse's Reversal of Fortune | History & Archaeology |". Smithsonian Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-04-19. Iliwekwa mnamo Novemba 26, 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)