Radi (elementi)
Kwa ngurumo ya umeme tazama radi
Radi | |
---|---|
Jina la Elementi | Radi |
Alama | Ra |
Namba atomia | 88 |
Uzani atomia | 226,0254 u |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 18, 8, 2 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 973 K (700 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2010 K (1737 °C) |
Radi (kutoka Kilatini "radius") ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Ra.
Namba atomia ni 88 na uzani atomia ni 226.0254.
Jina limechaguliwa kutokana na tabia yake ya ununurifu: kwa Kilatini "radius" yamaanisha "mwale" au "mwonzi".
Kikemia radi ni metali ya udongo alikalini yenye rangi nyeupe. Lakini inaoksidisha haraka kushika rangi nyeusi.
Radi ni haba sana hutokea kama sehemu ya mchanganyiko wa madini kadhaa pamoja na urani. Hutokea hasa kama isotopi ya 226Ra yenye nusumaisha ya miaka 1,602 ikibadilika kuwa gesi ya radoni.
Historia ya radi
[hariri | hariri chanzo]Radi ilitambuliwa mara ya kwanza mwaka 1898 na mwanakemia Mpolandi Marie Curie na mume wake Mfaransa Pierre. Baadaye ilitumiwa kwa ajili ya saa zilizotakiwa kuonekana usiku kwa sababu radi inang'aa gizani kutokana na unururifu wake. Ilitumiwa pia kama dawa hadi ilipoonekana mnamo 1930 ya kwamba inasababisha magonjwa ya kansa.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Radi (elementi) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |