Nenda kwa yaliyomo

Radi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa maana tofauti ya neno hili kama elementi ya kikemia angalia radi (elementi)

Radi nchini Marekani

Radi (pia: ngurumo ya umeme) ni mwangaza na miale ya mwanga mithili ya shoti za umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga katikati ya mawingu unaweza kuitwa "umeme".

Matumizi ya neno "umeme" kwa ajili ya teknolojia ya "stimu" (jinsi electricity inavyoitwa nchini Kenya) na vifaa vya umeme yamesababisha kukaza tofauti kati ya umeme kwa jumla na kutokea kwake kwa ghafla wakati wa mvua kali kama mwangaza mkali. Hata hivyo maana asili ya "umeme" ni ule mwangaza.

Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hiyo ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani unaoonekana kama mwangaza mkali. Mkondo unatoa pia joto kali na joto hilo husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huo unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali, lakini inaweza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu.

Kama mwendo wa radi ni kutoka mawinguni kwenda ardhi unaweza kuleta hasara kwa watu au vitu. Takriban watu 2,000 hupigwa na radi kila mwaka na mara nyingi wanakufa. Radi huwasha moto kwenye nyumba au pori.

Radi inayolenga ardhi huelekea kuingia sehemu ya juu mahali inapopiga. Hapo kuna mitambo ya kikingaradi [1]: ni chuma zilizopo juu ya dari ya nyumba na kuendelea hadi ndani ya ardhi kando ya nyumba. Kama radi inapiga nyumba itachukua njia ya haraka ya kufika ardhini kwa hiyo itapita kwenye vyuma bila kuharibu nyumba yenyewe.

Tofauti ya madhara yaliyopo kati ya radi na ngurumo hutegemeana na kiwango cha athari zinazojitokeza. Kwa kuwa ule wa radi ni umeme mkubwa sana, hivyo basi madhara yake ni makubwa sana kulinganisha na sauti kubwa na ya kuogofya inayotokea muda mfupi tu baada ya radi kutokea.

  1. An earth wire is literally a wire that goes down into the earth - also known as an “earth ground.” It's meant to be the electrical path that unwanted electricity (such as lightning or a short-circuit) finds easiest to take.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Radi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.