Nenda kwa yaliyomo

Murti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Murti ya mungu Venkateswara

Murti ni neno la Kisanskrit ambalo linamaanisha sanamu ya mungu fulani katika dini ya Uhindu[1]. Kwa imani ya Kihindu murti si mungu mwenyewe bali ishara yake ambamo roho ya mungu inajionyesha[2].

Waumini Wahindu huombea kuwepo kwa mungu katika sanamu ili waweze kuwasiliana naye na kupokea baraka zake. Wahindu hawaziabudu murti au sanamu yenyewe bali mungu ambaye yuko katika roho zao. Murti hupatikana hekaluni lakini ziko pia nyumbani mwa Wahindu wengi kwa matumizi ya ibada.[3]

Nafasi ya murti katika ibada

Katika Uhindu, mwumini hutazama ndani yake na kupitia sanamu ya Shiva ili kumwita mungu katika mwili wake wa kiroho.
Murti ya mungu Ganesha

Murti mara chache hupatikana bila umbo maalumu lakini kwa kawaida ni sanamu za mawe au metali zinazomwonyesha mungu fulani katika umbo la kibinadamu kama vile Shiva au Ganesha, Rama au Krishna, Saraswati au Kali.

Murti huchongwa kulingana na maagizo madhubuti na kisha kuwekwa hekaluni na makuhani wenye mafunzo katika ibada maalumu.

Marejeo

  1. PK Acharya, An Encyclopedia of Hindu Architecture, Oxford University Press, page 426
  2. Jeaneane D Fowler (1996), Hinduism: Beliefs and Practices, Sussex Academic Press, ISBN 978-1-898723-60-8, pages 41–45
  3. James Lochtefeld (2002), The Illustrated Encyclopedia of Hinduism: A-M, The Rosen Publishing Group, ISBN 978-0-8239-3180-4, page 726