Mikoa ya Kamerun
Mandhari
Mikoa ya Kamerun ni maeneo ya utawala wa ngazi ya juu nchini Kamerun. Kwa lugha ya Kifaransa huitwa "région" tangu mwaka 2008 ambapo rais Paul Biya alibadilisha jina rasmi kutoka "provinces" za awali kuwa "régions. Jumla ya mikoa ni 10.
Mikoa hiyo hugawiwa katika wilaya (kwa Kifar. départements) 58. Ndani ya wilaya kuna tarafa (arrondissements) 360, manispaa (municipalités) na maeneo ya kichifu (chefferies).
Kila mkoa uko chini ya mkuu wake anayeitwa gavana (gouverneur de région) na kuteuliwa na rais wa jamhuri, pamoja na Halmashauri ya Mkoa.
Halmashauri ya Mkoa ni serikali ya mkoa. Ina wawakilishi wa wilaya wanaochaguliwa na wawakilishi wa watawala wa jadi:
- Mkoa wa Adamawa Adamawa,
- Mkoa wa Kati (Centre),
- Mkoa wa Mashariki (Est),
- Mkoa wa Kaskazini ya Mbali (Extreme Nord),
- Mkoa wa Pwani (Littoral),
- Mkoa wa Kaskazini (Nord),
- Mkoa wa Kaskazini-Magharibi (Nord-Ouest),
- Mkoa wa Magharibi (Ouest),
- Mkoa wa Kusini (Sud), na
- Mkoa wa Kusini-Magharibi (Sud-Ouest)