Nenda kwa yaliyomo

Mapigano ya Lepanto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapigano ya Lepanto yalivyochorwa mwishoni mwa karne ya 16.

Mapigano ya Lepanto yalifanyika baharini tarehe 7 Oktoba 1571 kati ya manowari za nchi za Kikristo za Bahari Mediteranea na Milki ya Osmani, zilipokutana katika Ghuba ya Patras (karibu na Ugiriki). Lepanto ni jina la bandari zilipoondoka meli za Waosmani, wakati zile za mshikamano wa Kikristo zilitokea Messina (Italia).

Kwenye mwaka 1570 Waosmani walivamia kisiwa cha Kupro kilichotawaliwa na Venezia na mwaka 1571 walifaulu kuteka ngome ya mwisho iliyotetewa na Venezia.

Mwaka uleule wa 1571 Papa Pius V aliunganisha nchi za Kikatoliki kadhaa, hasa Hispania, jamhuri za Venezia na Genova na madola madogo ya Italia katika "Liga Sancta" ili kuzuia Waturuki wa dola hilo wasiteke Ulaya nzima. Ujerumani iliyowahi kufanya mapatano ya amani na Waosmani na Ufaransa iliyoshiriki na Waosmani dhidi ya Hispania hawakushiriki katika Liga Sancta.

Kundi la manowari la Kiosmani lilikuwa na manowari aina ya manchani 255 Galeeren, askari 34,000 Soldaten na mabaria na wapiga makasia 46,000, wakati kundi la Liga Santa lilikuwa na manchani 206 Galeeren, askari 28,000 Soldaten na mabaharia na wapiga makasia 40,000.

Ingawa jeshi la baharini la Wakristo lilizidiwa na jeshi la Dola la Osmani kwa idadi, walipata ushindi mkubwa. Matokeo yake yakawa ya kudumu: Waturuki hawakuweza kuteka Ulaya magharibi[1] wala kwenda Amerika kupitia bahari ya Atlantiki.

Ushindi huo haukutegemewa, ila uliombwa na Wakatoliki wa Ulaya nzima kwa Rozari, kama alivyoagiza Papa[2][3]. Pius V aliona ushindi huo umetokana na maombezi ya Bikira Maria akaanzisha sikukuu ya Bibi Yetu wa Ushindi. Mjini Roma mwenyewe aliongoza maandamano ya ibada kwa ajili hiyo.

  1. "Melleuish, Gregory. "The significance of Lepanto", Quadrant, April 1, 2008". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-06-29. Iliwekwa mnamo 2017-06-07. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  2. Chesterton, Gilbert.Lepanto, Ignatius Press, 2004, ISBN 1-58617-030-9
  3. Butler's Lives Of The Saints (April) by Alban Butler (1999) ISBN 0-86012-253-0 page 222
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapigano ya Lepanto kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.