Nenda kwa yaliyomo

Kipindi cha kujizungusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katika elimuanga, kipindi cha kujizungusha ni muda ambapo gimba linajizungusha mara moja kwenye mhimili wake. Kuna jinsi mbili za kupima kipindi cha kujizungusha. Jinsi moja ni sawa na siku ya jua, yaani siku kawaida (saa 24 duniani). Jinsi nyingine ni sawa na siku ya nyota, yaani muda ambapo nyota za mbali zinarudia mahali palepale angani (saa 23.9344696 duniani). Aina hizi mbili za siku zinatofautiana kwa kuwa mwendo wa Dunia kuzunguka Jua husababisha kwamba nyota za mbali zinaenda angani polepole kuliko Jua. Kwa kanuni, vitu vya mbali vinaenda polepole kuliko vitu vya karibu. Kwa mfano, ukiendeshea gari, milima ya mbali inaonekana kama kwamba inaenda polepole sana kuliko miti ya karibu. Kwa athari hiyohiyo, mahali pa nyota na mahali pa Jua huwa panatofautiana kwa nyuzi 1 ya ziada kila siku. Siku ya jua ni ile iliyoonekana zaidi duniani; sisi wote tunaona kwa muda gani kuna Jua, na kwa muda gani kuna giza ya usiku. Lakini kuangalia siku ya nyota ni kugumu zaidi. Hivyo kwa watu wengi siku ya jua ni aina pekee ya siku wanayojua.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kipindi cha kujizungusha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.