Kioksitania
Kioksitania ("occitan") ni lugha ya jimbo la Katalunya ya magharibi ya kaskazini, Ufaransa wa kusini, Italia ya magharibi ya kaskazini na ya kusini, Monaco. [1]
Pia inajulikana kama
[hariri | hariri chanzo]Occitan, Lenga d'òc
Idadi ya wasemaji (takriban)
[hariri | hariri chanzo]Toka 1.000.000 mpaka 3.700.000
Katalunya ya magharibi ya kaskazini (4.000), Ufaransa wa kusini (toka 1.000.000 mpaka 3.600.000), Italia ya magharibi ya kaskazini na ya kusini (toka 50.000 mpaka 100.000), Monaco (4.500).
Cheo halali
[hariri | hariri chanzo]Rasmi pamoja na nyingine. Katalunya ya magharibi ya kaskazini. Haijakubaliwa: Ufaransa wa kusini. Imekubaliwa halali: Italia ya magharibi ya kaskazini na ya kusini.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Matumizi ya Occitan kama lugha ya serikali na ya vitabu yaliimarishwa mwanzo wa wakati wa Middle Ages. Maandiko ya kwanza, mwanzo wao ulikuwa karne 11. Kwenye karne 12 na 13 lugha ilipata nguvu sana ndani ya Ulaya. Lakini baadaye Ufaransa ulianza kutawala kwa nguvu nchi nzima na Kifaransa kilianza kutumiwa na watu wa Occitania.
Kumekuwa na majaribio ya kusitawi lugha tena, hasa kwenye vipindi fulani vya nusu ya pili ya karne 19 na karne 20 Ulaya. Matokeo ya hayo majaribio yamekuwa kuipatisha lugha cheo cha juu baina ya lugha za vitabu vyenye ufasaha Ulaya, na kuiingiza lugha katika shule, magazeti, redio, televisheni, na kadhalika. Vilevile imewekwa lahaja sanifu, yenye asili ya lahaja za Languedoc lakini yenye michango iliyotolewa kwa lahaza nyingine zote.
Tawi moja la lahaja za Occitan linaitwa Gasconian, na lina lahaja moja inayoitwa Aranese, ambayo eneo lake ni bonde la Aran, lililo sehemu moja ya Katalunya tangu karne 14. Katalunya ina sheria zake zenyewe, tofauti na zile za sehemu nyingine za Uhespanyola. Mkusanyo wa sheria za Katalunya unaitwa Estatut d'Autonomia de Catalunya. Kwa sababu ya hizo sheria, Aranese ilitunzwa na kuimarishwa, ikapata cheo cha rasmi mwaka 1990, pamoja na Kikatalani na Kihespanyola.
Kabla ya wakati huu, uandikaji ulirekebishwa (1982) kwa njia ambayo ilimaanisha kukubali na kuonyesha wazi kwamba Aranese ndiyo lahaja ya Occitan; na matumizi yake shuleni yalianza mwaka 1984. Siku za leo Aranese ni lugha ya serikali, ya elimu, na ya waandishi (wa habari na wa vitabu). Njia ya upotevu wa Occitan kwa kuweka Kifaransa badala yake, ambayo inatukia Ufaransa, haijageuza lahaja ya Aranese, iliyo na nguvu na maisha mazuri, pamoja na mikusanyiko ya watu wa vyama fulani wanaoihifadhi. Hata hivyo, hali yake nzuri haijaimarishwa kabisa na ina hatari na kuingia katika njia ya upotevu kwa sababu ya Kihespanyola na Kikatalani, lugha ambazo zinajulikana na watu wengi wa bonde la Aran na ambazo zinazungumzwa na baadhi kubwa ya watalii na wahamiaji wanaofika pale kila mwaka.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- makala za OLAC kuhusu Kioksitania
- lugha ya Kioksitania katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/oci
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-19. Iliwekwa mnamo 2008-09-18.