Kifukofuko
Mandhari
Kifukofuko ni kiganda cha nyuzi asilia inayotolewa na mabuu (viluwiluwi) ya wadudu mbalimbali kama vile vipepeo. Kusudi lake ni kujikinga hadi kufikia hatua ya maendeleo yao inayofuata. Buu latoa kioevu kinachoganda hewani kuwa uzi. Lajiviringisha katika uzi hiyo hadi limefunikwa na kukingwa kabisa nayo.
Uzi hiyo huitwa "hariri" na kutokana na aina ya mdudu inatokea kama ganda laina kama vile hariri ya kitambaa au ngumu kabisa.
Ndani ya kifukofuko mdudu anabadilika hadi kutokea. Kwa mfano mdudu katika hali ya kivawi ajifunga ndani na kutoka kama kipepeo baada ya muda unaotegemea na aina yake; muda mfupi ni wiki mbili lakini katika nchi za baridi mdudu hulala ndani ya kifukofuko chake kwa miezi kadhaa.